Alexander Bastrykin
Alexander Ivanovich Bastrykin (alizaliwa 27 Agosti 1953) ni mwanasheria wa Urusi ambaye anahudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi ya Urusi tangu tarehe 15 Januari 2011. Awali alihudumu kama Naibu Mkuu wa Kwanza wa Mwanasheria Mkuu wa Urusi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.
Ana cheo maalum cha Jenerali wa Sheria (General of Justice), cheo cha kitaaluma cha Profesa, na Udaktari wa Sayansi|shahada ya uzamivu katika sheria.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Alexander Bastrykin alihitimu kutoka Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Serikali cha Leningrad mnamo mwaka 1975, na alikuwa mwanadarasa mmoja wa chuo kikuu na Vladimir Putin.[1][2][3]
Mnamo mwaka 2007, Rais Vladimir Putin alianzisha Kamati ya Uchunguzi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ambayo de facto (kwa uhalisia) ilikuwa huru kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, na Bastrykin akawa mwenyekiti wake wa kwanza. Inaripotiwa kuwa uteuzi huo ulichochewa na Igor Sechin, aliyetaka kulinda ushawishi wake baada ya mshirika wake wa karibu Vladimir Ustinov kuondolewa katika nafasi ya mwanasheria mkuu mnamo mwaka 2006.[1][2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 "Бастрыкин, Александр". Iliwekwa mnamo 26 Machi 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "Однокашник президента возглавит прокурорское следствие". Коммерсантъ: 6. 22 Juni 2007. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2018 – kutoka Kommersant.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "Сечинский комитет при Генпрокуратуре". Политком.RU: информационный сайт политических комментариев. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alexander Bastrykin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |