Nenda kwa yaliyomo

Aleksandr Solzhenitsyn

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Solzhenitsyn, 1994
One Day in the Life of Ivan Denisovich

Aleksandr Isayevich Solzhenitsyn (11 Desemba 19183 Agosti 2008) alikuwa mwandishi na mwanahistoria kutoka nchi ya Urusi.

Mwaka wa 1970 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Anajulikana hasa kwa kitabu chake "Funguvisiwa la Gulag" (kwa Kirusi Arkhipelag Gulag) kilichotolewa katika majuzuu matatu miaka ya 1973-75. Katika kitabu hicho alisimulia historia ya utawala wa kutisha wa Stalin na mfumo wa makambi yake mengi kwa wafungwa wa kisiasa. Alikamatwa na serikali na kufukuzwa nje ya nchi kwa sababu ya kitabu hicho.

Mwaka wa 1994 alirudi Urusi. Aliaga dunia Moscow mjini mwaka wa 2008.

Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aleksandr Solzhenitsyn kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.