Aleksanda wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aleksanda wa Konstantinopoli (264 hivi - 337 hivi) alikuwa askofu wa Bizanti, baadaye askofu mkuu wa kwanza wa mji huo kwa jina jipya la Konstantinopoli, leo Istanbul nchini Uturuki, kuanzia mwaka 314 hadi kifo chake[1].

Inasemekana kwanza alikuwa mmonaki kutoka Calabria, Italia Kusini.

Alipinga kwa nguvu zote Uario bila kujali vitisho wa kaisari Konstantino Mkuu na wengineo[2].

Gregori wa Nazianzo aliandika kuwa Aleksanda alishinda uzushi huo kwa sala zake[3].

Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tangu kale kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Agosti[4] au 30 Agosti.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/67850
  2. Kazhdan, Alexander; Talbot, Alice-Mary (2005-01-01). "Constantinople, Patriarchate of". The Oxford Dictionary of Byzantium. Oxford University Press. ISBN 978-0-19-504652-6. Iliwekwa mnamo 2018-07-25.
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/67850
  4. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.