Alda Lara
Alda Lara alizaliwa tarehe 9 1930 katika mji wa Benguela Angola Ureno. Alitokea katika familiya ya kitajiri na alipata elimu ya Kikristo, ambayo ilimpa uhuru wa nafsi kulingana na mchambuzi. Kaka yake alikuwa mshairi mashuhuri aliyeitwa Ernesto Lara Filho . Lara alisoma katika shule ya wanawake huko (kwa sasa inafahamika kwa jina la Lubango) Sá da Bandeira, kabla ya kuhamia Ureno kumaliza shule ya sekondari. [1] Alisoma katika Chuo Kikuu cha Lisbon na akaishi katika Nyumba ya Wanafunzi wa Dola. Alikuwa mwanafunzi mwenye bidii na alianza kazi yake ya uandishi kwa kuchapisha mashairi katika jarida la kifasihi Mensagem, chapisho mahususi kwa Waafrika. Baadaye Lara alienda kusoma katika Chuo Kikuu cha Coimbra na kupata digrii katika masuala ya dawa.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Biografia de Alda Lara". Lusophonia Poetica (kwa Portuguese). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Sheldon, Kathleen (2016). Historical Dictionary of Women in Sub-Saharan Africa (tol. la 2nd.). Rowman & Littlefield. uk. 155. ISBN 978-1442262935.