Alberto wa Pontida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Alberto wa Pontida.

Alberto wa Pontida, O.S.B. (Prezzate, 1025; † 2 Septemba 1095), alikuwa abati huko Lombardia, Italia.

Alberto alikuwa kati ya wamonaki waliojitahidi zaidi kueneza urekebisho wa Cluny katika mkoa huo. Hata hivyo, alikuwa upande wa kaisari Henri IV wa Ujerumani katika mashindano yake na Papa Gregori VII.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Septemba[1] pamoja na mwenzake Vito[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kabla hajajiunga na umonaki, alikuwa askari kufuatana na kawaida ya koo maarufu za wakati huo. Ni baada ya kujeruhiwa sana vitani kwamba aliamua kufuata maisha ya Kiroho badala ya kulenga tena ushindi na heshima ya kidunia[3].

Alipokwenda kuhiji Santiago de Compostela (Hispania) alipitia monasteri kadhaa za Waklunii na kuvutiwa sana na maisha ya namna hiyo.

Aliporudi nyumbani alijitolea mali yake kuanzisha monasteri (1059).

Baadaye alikwenda kupata malezi ya Hugo wa Cluny kwa miaka saba.

Tena akarudi Pontida kuongoza monasteri yake na kuanzisha nyingine kwa wanawake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/69310
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/69300

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • G.M. Cantarella, I monaci di Cluny, Einaudi, Torino, 1997;
  • J. Huizinga, L'autunno del Medioevo, Newton-Compton, Roma, 1997;
  • J. Le Goff, L'uomo medievale, Laterza, Bari, 1999;
  • Cognomi e famiglie del bergamasco, S.E.S.A.A.B., Bergamo, 2000
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.