Alberto Setele
Mandhari
Alberto Setele (22 Novemba 1935, Zavala – 7 Septemba 2006) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Msumbiji na Askofu wa Jimbo Katoliki la Inhambane.
Alipadrishwa tarehe 9 Agosti 1964. Mnamo 20 Novemba 1975, Papa Paulo VI alimteua kuwa Askofu wa Inhambane. Alipokea daraja ya uaskofu tarehe 8 Februari 1976 kutoka kwa Askofu Mkuu wa Maputo, Alexandre José Maria dos Santos, akisaidiwa na Maaskofu Ernesto Gonçalves da Costa wa Beira na Januário Machaze Nhangumbe wa Pemba.
Alifariki dunia tarehe 7 Septemba 2006 akiwa na umri wa miaka 70.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Bishop Alberto Setele †". Catholic-hierarchy.org. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |