Nenda kwa yaliyomo

Alba Flores

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alba Flores

Alba González Villa (alizaliwa 27 Oktoba 1986), anayejulikana kitaaluma kama Alba Flores, ni mwigizaji wa Kihispania. Anajulikana zaidi kwa nafasi ya Saray Vargas katika tamthilia ya uhalifu inayohusu maisha gerezani ya Vis a Vis (2015–2019), na nafasi ya Nairobi katika tamthilia ya wizi ya Money Heist (2017–2021).

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Flores ni binti wa mwanamuziki na mtunzi wa muziki Antonio Flores na Ana Villa, ambaye ni mtayarishaji wa michezo ya jukwaani. Familia yake inajumuisha wasanii wa maonyesho, wanamuziki na waigizaji wenye asili ya Waromani. Yeye ni mjukuu wa Lola Flores, aliyejulikana kwa jina la “La Faraona” (“Farao wa Kike”), mpwa wa waimbaji Lolita Flores na Rosario Flores, na binamu wa mwigizaji Elena Furiase.

Babu yake kwa upande wa baba, Antonio González, aliyejulikana kama “El Pescaílla”, pia alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa wa Kihispania. Anahesabiwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa Catalan Rumba.[1][2]

  1. ↑ https://www.imdb.com/name/nm1699346/
  2. ↑ https://www.infobae.com/parati/news/2018/01/28/tokio-nairobi-las-actrices-espanolas-que-la-rompen-en-la-casa-de-papel/
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alba Flores kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.