Nenda kwa yaliyomo

Alan Marshall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Alan Marshall')

Alan Marshall (amezaliwa 1975) ni mwandishi, msomi na msanii kutoka Australia[1] anayejihusisha na masuala ya mazingira, hususan maadili ya mazingira na miji rafiki kwa mazingira ya baadaye,[2]

Miradi Yake Mikubwa

[hariri | hariri chanzo]

Alianzisha Mradi wa Ecomimicry mwaka 2006 uliounganisha ekolojia na uvumbuzi[3], na baadaye mwaka 2013 akaanzisha Mradi wa Miji ya Kijani ya Baadaye ulibuni taswira za miji 100 duniani, uliopokelewa na kuchapishwa katika kitabu chake mashuhuri Ecotopia 2121.[4] Kazi zake zimeonyeshwa kwenye makumbusho kama Bauhaus na Museum of London na kushinda tuzo mbalimbali, zikiwemo Nautilus Book Awards na Green Book Festival. Pia ameandika kitabu kama Wild Design chenye ubunifu wa miundo rafiki kwa mazingira, na kitabu The Unity of Nature ambacho kilikosoa vikali nadharia za kisayansi kama Gaia na Chaos.[5]

Mbali na miradi hiyo, Marshall alianzisha Frankencities mwaka 2015 akionyesha hali mbaya zaidi za mazingira katika miji kwa kuhusisha simulizi ya Frankenstein, na kubuni Mbinu ya Kifasihi ya Usanifu Miji iliyolenga mikakati ya mabadiliko ya kijamii.[6] Mnamo 2020, alianzisha Global Sheeplands kuchunguza mchango wa ufugaji kondoo katika historia ya dunia. Pia ni mkosoaji wa sekta ya magari, nyuklia na tafiti za anga za juu, akisisitiza ulinzi wa mazingira ya sayari.[7] Mbali na taaluma, Marshall ameandika riwaya na tamthilia za redio kama 'This Pointless Thing Called Life' na 'This Miserable Thing Called Life', ambazo zilipata tuzo na kutangazwa Marekani[8]. Kazi zake zote za kifasihi na kitaaluma zimebaki zikichunguza uhusiano kati ya binadamu, teknolojia na mazingira.

  1. Oliphant, Jill (2011). AQA religious ethics for AS and A2. Jon Mayled, Anne Tunley. London: Routledge. ISBN 978-0-203-83021-5.
  2. Christopher Sandom, Jo Walton (2024-09-20). "Our 24-hour climate comic explores what a sustainable future could look like". doi.org. Iliwekwa mnamo 2025-09-04.
  3. doi.org https://doi.org/10.17658/issn.2058-5462/issue-19/rstratton/abstract. Iliwekwa mnamo 2025-09-04. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)
  4. Marshall, A. (2016-12-21). "These six utopian cities of the future will help you re-imagine life on Earth". doi.org. Iliwekwa mnamo 2025-09-04.
  5. Marshall, Alan (2002). The Unity of Nature - Wholeness and Disintegration in Ecology and Science. Imperial College Press. ISBN 978-1-86094-954-8.
  6. Franziska Mey, Chris Briggs (2018-11-27). "What would a fair energy transition look like?". doi.org. Iliwekwa mnamo 2025-09-04.
  7. Marshall (2014). "Ecotopia 2121 AD: Sustainable Cities of the Future". Resilience: A Journal of the Environmental Humanities. 1 (2). doi:10.5250/resilience.1.2.003. ISSN 2330-8117.
  8. Furth, David; Chair, Committee (2013-03). "The Coleopterists Society Youth Incentive Awards". The Coleopterists Bulletin. 67 (1): 22–22. doi:10.1649/072.067.0104. ISSN 0010-065X. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)