Utambulisho wa nchi
Mandhari
(Elekezwa kutoka Alama ya Nchi)
Utambulisho wa nchi ni aina ya alama inayowekwa inayojuulikana kama chanjo ya ngozi (scarification) iliyokuwa ikionekana kwa watumwa waliofika Amerika Kaskazini katika karne ya 18 na ya 19 kama sehemu ya Biashara ya utumwa kupitia Atlantiki[1] .
Alama hizo za nchi zilitumika sana kuwatambulisha watumwa mmojammoja, na mara nyingi zilitajwa katika matangazo ya magazeti yaliyotafuta watumwa waliotoroka.
Wanahistoria wa biashara ya watumwa wametumia alama hizo za mwilini kutambua asili au taifa la watumwa hao, hasa pale ambapo kumbukumbu za maandishi hazikuonyesha walikotoka.[2]