Nenda kwa yaliyomo

Al-Kahf

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sura 18 katika Quran
الْكَهْف
Al-Kahf
Pango

﴿١﴾ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجًا ۛ
﴿٢﴾ قَيِّمًا لِّيُنذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا mِّن لَّdُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا
...
Sikiliza kisomo cha sura hii
MapokeoMakka
Juzuu15–16
Idadi ya Aya110
Idadi ya Maneno1,583
Idadi ya Herufi6,425
17: Al-Isra'19: Maryam

Al-Kahf (kwa Kiarabu: الكهف al-Kahf, maana: "Pango") ni sura ya 18 katika mpangilio wa msahafu wa Qurani, kitabu cha dini ya Uislamu. Sura hii ina jumla ya aya 110 na inatambulika kuwa ni sura ya Makka (Makkiyyah) kwa sababu ilishushwa kabla ya Hijrah ya Mtume Muhammad kwenda Madina.[1]

Sura hii inashikilia nafasi ya upekee katika maisha ya kila wiki ya Waislamu, inashauliwa kwa kuwa ni miongoni mwa Sunna katika mapokeo ya hadithi kusoma sura hii kila siku ya Ijumaa kwa ajili ya kupata mwongozo wa kiroho na kinga dhidi ya fitna za Masihi Dajjal.[2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Inaelezwa kuwa jina la sura hii linatokana na kisa cha kwanza kilichotajwa ndani yake kuanzia aya ya 9 hadi ya 26 kinachohusu "Watu wa Pangoni". Kisa hiki kinahusu vijana waliokimbia mji wao kulinda imani yao dhidi ya mfalme dhalimu, ambapo walijificha pangoni na kulazwa usingizi na Mwenyezi Mungu kwa muda wa zaidi ya miaka 300 pamoja na mbwa wao aliekuwa mlangoni.

Mbali na kisa hicho, sura hii inakusanya jumla ya visa vingine vitatu vikuu vya kihistoria vyenye mafundisho tofauti: kisa cha pili ni cha mtu aliyejivunia utajiri wa bustani zake mbili na kukata tamaa na neema za kimungu, kikifundisha umuhimu wa unyenyekevu; kisa cha tatu ni safari ya kihistoria kati ya Nabii Musa na mja mwema Khidr inayobainisha siri za hekima na elimu ya kimungu katika matukio ya kimaisha; na kisa cha nne ni cha mfalme muadilifu, Dhul-Qarnayn, aliyezunguka dunia kusimamisha uadilifu na kujenga ukuta mkubwa wa chuma ili kuzuia uharibifu wa jamii za Yajuj na Majuj.[3]

  1. Bosworth, C.E. (1997). Encyclopedia of Islam, Second Edition. Juz. la 4. Brill. ku. 407–408. Iliwekwa mnamo Mei 22, 2026.
  2. "Sahih Muslim - Virtues of Surah Al-Kahf and Dajjal". Sunnah.com Portal. Iliwekwa mnamo Mei 22, 2026.
  3. Farsy, Abdullah Saleh (1969). Tafsiri ya Kurani Tukufu. The Islamic Foundation. Iliwekwa mnamo Mei 22, 2026.