Akatistos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akatistos kwa lugha ya Kislavi cha Kikanisa. Oikos One.
Picha takatifu ya Theotokos akisali, Kanisa kuu la Spasky, Yaroslavl (karne ya 13).
Akatistos ya Theotokos. Sehemu ya mchoro wa ukutani, 1644, Kremlin, Moscow, Urusi.

Akatistos (kwa Kigiriki: Ἀκάθιστος Ὕμνος, "utenzi usiotaka ukae"[1]) ni utenzi wa Ukristo wa mashariki kwa nafsi mojawapo ya Utatu Mtakatifu, kwa tukio fulani la kalenda ya liturujia, au kwa mtakatifu yeyote.

Akatistos ya Bikira Maria[hariri | hariri chanzo]

Akatistos maarufu zaidi ni ile iliyoandikwa katika karne ya 7 kwa heshima ya Mama wa Mungu. Mtunzi wake hajulikani kwa hakika.

Kwa sasa imeenea hata katika Kanisa la magharibi na kuna tafsiri mbili katika lugha ya Kiswahili: moja ya Waorthodoksi wa Kenya, nyingine ya Wakatoliki wa Tanzania.

Pia, kuna picha takatifu za Theotokos zinazojulikana kwa jina "Akatistos".

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. The name derives from the fact that during the chanting of the hymn, or sometimes the whole service, the congregation is expected to remain standing in reverence, without sitting down (ἀ-, a-, "without, not" and κάθισις, káthisis, "sitting"), except for the aged or infirm.

Matini kwa Kigiriki[hariri | hariri chanzo]

  • G. Papagiannis, Ακάθιστος Ύμνος. Άγνωστες πτυχές ενός πολύ γνωστού κειμένου. Κριτικές και μετρικές παρατηρήσεις, σχολιασμένη βιβλιογραφία. Thessaloniki 2006.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]