Aiwanose Odafen
Aiwanose Odafen ni mwandishi wa Nigeria mwenye mwelekeo wa kifeministi. Anajulikana zaidi kwa riwaya zake Tomorrow I Become a Woman (2022) na We Were Girls Once (2024).
Alizaliwa mjini Lagos, Nigeria. Alisoma katika Nigerian Turkish International Colleges na alihitimu mwaka wa 2009. Mwaka wa 2013 alihitimu Shahada ya Sayansi katika uhasibu (Accounting) katika Chuo Kikuu cha Covenant.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Odafen alizaliwa Lagos, Nigeria. Alipata elimu yake ya sekondari katika Nigerian Turkish International Colleges. Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Covenant, ambapo alisomea uhasibu na kuhitimu mwaka 2013.
Mwaka 2015 alipata Shahada ya Uzamili wa Biashara (MBA) katika Chuo Kikuu cha Oxford. Baadaye alipata Shahada ya Uzamili ya Uandishi Bunifu (MFA) katika Iowa Writers’ Workshop mwaka 2024. Pia alihudhuria warsha ya uandishi ya Chimamanda Ngozi Adichie iitwayo Purple Hibiscus Trust Writing Workshop. Hadithi yake fupi Faces iliorodheshwa katika tuzo ya Commonwealth Short Story Prize mwaka 2020.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Odafen ni mhasibu kitaaluma na ni mwanachama wa Association of Chartered Certified Accountants (ACCA) nchini Uingereza. Amefanya kazi katika sekta ya uhasibu sambamba na uandishi.
Mnamo Mwaka wa 2020, riwaya yake ya kwanza Tomorrow I Become a Woman ilichukuliwa na Scribner UK, kampuni tanzu ya Simon & Schuster UK, na ilichapishwa mwaka wa 2022. Pia Kitabu hicho kiliorodheshwa katika orodha mbalimbali za vitabu bora vya Afrika, ikiwemo Brittle Paper 100 Notable African Books of year 2022, Open Country Mag 60 Notable Books of year 2022, na Afrocritik Top 25 African Novels of year 2022.
Mnamo Mwaka wa 2022 alichangia katika mkusanyiko wa hadithi I Am Adona, unaoangazia wanawake wa Afrika na mafanikio yao katika haki na uwezeshaji wa wanawake.
Riwaya yake ya pili We Were Girls Once ilichapishwa tarehe 25 mwezi Aprili mwaka wa 2024. Kitabu hicho kimeelezwa na wakosoaji kama kazi iliyo “kali, isiyo na mapambo na yenye nguvu ya kihisia”.
Bibliografia
[hariri | hariri chanzo]- Tomorrow I Become a Woman (2022)
- We Were Girls Once (2024)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aiwanose Odafen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |