Aishatu Madawaki
Aishatu Madawaki MFR, MFR (alizaliwa 1961) ni mwanamke msomi na mwanasiasa kutoka Nigeria. Yeye ni profesa wa kwanza mwanamke kutoka majimbo ya zamani ya ukhalifa ya Sokoto (lenye kujumuisha Jimbo la sasa la Sokoto, Jimbo la Zamfara na Jimbo la Kebbi ), mahali ambapo Waislam wengi wanaishi Kaskazini mwa Nigeria . Mwaka wa 1999, alipewa nafasi ya kamishna wa masuala ya wanawake na maendeleo ya jamii na uongozi uliyosimamiwa na Attahiru Bafarawa. Madawaki anahusika na ni mtetezi pia wa uwakilishi wa wanawake wa Nigeria kwnye siasa.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Mahali alipozaliwa ni Gusau, kisa Madawaki alipata masomo ya shule ya msingi kwenye Shule ya Msingi ya Sarkin Kudu. [1] Baada ya hapo akapata masomo yake ya Sekondari ndani ya Shule ya Upili ya Wasichana ya Serikali, Kotarkoshi. Alifanikiwa kupata Cheti chake cha Kitaifa cha Elimu kutoka Chuo cha Elimu, Sokoto (lenye jina jipya la Chuo cha Elimu cha Shehu Shagari ). Programu yake ilivyomalizika shuleni, alianza kufundisha saikolojia ya elimu kwenye taasisi hiyo hiyo. Alipata shahada yake ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Usmanu Danfodio, kisha shahada yake ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Bayero .
Madawaki amefanikiwa kuwa profesa wa kwanza wa jinsia ya kike kwenye Jimbo la zamani la Sokoto huko nchini Nigeria, lenye jumla ya majimbo matatu ndani ya Nigeria ya leo.
Kazi ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Madawaki akichaguliwa kuwa kamishna wa masuala ya wanawake na maendeleo ya kijamii kwenye serikali ya Attahiru Bafarawa kati ya mwaka 1999 na mwaka 2003. Majukumu mengine ya tofauti aliyoyafanya kwenye nafasi za jimbo zima ni jumuishi na kuwa mwenyekiti, bodi ya Huduma kwa Walimu (mwaka 2004–mwaka 2007). Kwenye nafasi ya shirikisho, alichaguliwa kuwa mjumbe, Kamati ya Ufundi ya Rais ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini kati ya mnamo wa 2002 na mnamo wa 2004; mjumbe, Bodi ya Ufundi ya Rais Benki ya Rehani ya Shirikisho, Abuja (mwaka wa 2004– mwaka wa 2007), na mjumbe mshirika, Tume ya Udhibiti wa Miundombinu, Abuja (2008–2012). [2]
Mwaka wa 2014, aliteuliwa kuwa mjumbe mwenye kutoa uwakilishi kwenye Jimbo la Sokoto kwenye mkutano mkuu wa kitaifa, mpango mikakati wa Rais Goodluck Jonathan wa kufumbua suluhu la kudumu kwa masuala yanayoinuka kwenye kuishi kwa pamoja kwa Wanigeria.
Mwaka wa 2017, aliunda maandamano ya amani kwenye Jimbo la Sokoto lenye kusudi la kutoa wito wa rais mwanamke ndani ya nchi ya Nigeria na kushinikiza uwakilishi zaidi wa wanawake ndani ya jimbo hilo. Hii ilifanya maafisa wa serikali ndani ya jimbo hilo kurudia kujitolea kwao kwenye usawa wa kijinsia ndani ya jimbo hilo. [3]
Kwenye tarehe ya Januari 2018, alichaguliwa kwenye afasi ya kamishna wa elimu ya msingi na sekondari kwa Jimbo la Sokoto na Gavana Aminu Waziri Tambuwal . Mwaka wa Aprili 2018, akiwemo pamoja na makamishna wengine 24 kwenye jimbo hilo, aliondolewa kazini na serikali kweye kile kilichoitwa na waajiri wake mantiki ya "kurekebisha na upangaji upya baraza la mawaziri kwa lengo la ufanisi bora na utoaji wa huduma kwa umma wa Jimbo".
Akizungumzia hoja ya ndoa kwa watoto wa umri katikati ya wanawake wa Kaskazini, Madawaki aliweka wazi kwamba ana wasiwasi zaidi juu ya mwelekeo wa familia ya wasichana kwakuwa na yeye aliolewa mapema sana japo wazazi wake walijua faida ya elimu na haikumzuia kuiendeleza. Kwenye mahojiano yaliyochapishwa na gazeti, Madawaki alichanga maoni yake kwamba kutengwa kwa wanawake kwa namna yoyote kunapaswa kuondolewa kibinadamu zaidi na sio kiholela wala kwakudhalilisha. Akiendelea kusema kwamba ingawa maagizo ya dini ya mtu yanazidi umoja wa kijinsia, wanawake hawapaswi kuzingatiwa kama walio chini ya wanaume, kwa sababu wakipewa fursa sawa katika nyanja fulani za maisha, wanaweza hata kufanya vizuri zaidi kuliko wenzao wa kiume. Alilaani ukabila na upendeleo katika nafasi ya kisiasa na kijamii ya Nigeria kama pia unawajibika kwa mgawanyiko wa kijinsia nchini Nigeria.
Madawaki amefanikiwa kupokea wa tuzo nyingi za kitaifa, MFR na OFR .
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "From the street to the classroom – Aisha's journey to an education".
- ↑ "Sokoto's first female professor sworn-in as commissioner". 16 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 2018-09-05.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nigeria: Sokoto Women Want Female Nigerian President". Premium Times. Iliwekwa mnamo 2018-09-05.