Aigulfi na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Visiwa vya Lerins.
Kanisa na monasteri ya Lérins.

Aigulfi na wenzake (walifariki kisiwa cha Capraia, leo nchini Italia, 676 hivi) walikuwa abati na wamonaki wenzake walioishi katika visiwa vya Lerins (leo nchini Ufaransa) na ambao waliuawa na maharamia Waislamu au na wamonaki waliokataa juhudi za uongozi wake [1].

Aigulfi (pia: Ayoul) alitokea Blois na kujiunga na monasteri ya Wabenedikto alipokuwa na umri wa miaka 20.

Kati ya wenzake, inasemekana 3 au 33, wanatajwa Turkari na Fronjenti.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Septemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.