Ahnenerbe (Urithi wa Wahenga)

Ahnenerbe (kwa Kijerumani: "Urithi wa Wahenga") lilikuwa shirika la kitafiti nchini Ujerumani lililoanzishwa mwaka 1935 na Heinrich Himmler, kiongozi wa kikosi cha SS, pamoja na Herman Wirth na Walther Darré. Ingawa lilijitangaza kama taasisi ya kisayansi ya kuchunguza historia ya kale ya utamaduni wa Kijerumani, lengo lake kuu lilikuwa la kisiasa na kikanuni chini ya Chama cha Nazi.[1] Shirika hili lilifanya kazi ya kutafuta uthibitisho wa kihistoria ili kuunga mkono nadharia za ubaguzi wa rangi za Wanazi, likidai kuwa watu wa "asili ya Kiarya" yaani Waarya walikuwa bora kuliko wengine wote duniani.[2]
Shirika hili lilitekeleza mradi wa kulazimisha utamaduni na mila za Kijerumani kwa njia ya ujanja, ambapo walibuni simulizi za uongo kudai kuwa mataifa mageni waliyotaka kuyavamia yalikuwa na asili au uhusiano wa damu na Wajerumani wa kale.[3] Kwa kutengeneza ushahidi wa bandia wa kihistoria, walijaribu kuhalalisha uvamizi wa nchi nyingine kama namna ya "kukomboa" ndugu zao waliopotea Ulaya hasa lakini mpaka Asia na Afrika pia.[4] Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Ahnenerbe ilijihusisha na vitendo vya kikatili, ikiwa ni pamoja na kufanya majaribio ya kinyama kwa binadamu katika kambi za mateso na kupora mali za kitamaduni ili kuthibitisha madai yao ya uongo kuhusu utukufu wa Ujerumani.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Michael Kater, Das "Ahnenerbe" der SS 1935-1945, 2006. (kwa Kijerumani)
- ↑ Heather Pringle, The Master Plan: Himmler's Scholars and the Holocaust, 2006. (kwa Kiingereza)
- ↑ David Barrowclough, Digging for Hitler: The Nazi Archaeologists Search for an Aryan Past, Fonthill Media, 2017. (kwa Kiingereza)
- ↑ Elizabeth R. Baer, The Genocidal Gaze: From German Southwest Africa to the Third Reich, Wayne State University Press, 2017. (kwa Kiingereza)
- ↑ Chapoutot, Johann (2014). La loi du sang : Penser et agir en nazi [Sheria ya damu: Kufikiri na kutenda kama Mnazi] (kwa Kifaransa). Gallimard.
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahnenerbe (Urithi wa Wahenga) Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |