Ahmed Umar
| Ahmed Umar | |
|---|---|
| Amezaliwa | Ahmed Umar 10/02/1988 |
| Utaifa | Sudan |
| Kazi yake | Msaani |
Ahmed Umar (Msanii) Ahmed Umar (kwa Kiarabu: أحمد عمر; alizaliwa Februari 10, 1988) ni msanii wa maonyesho na mwanaharakati wa haki za LGBT mwenye asili ya Sudan na Norway.[1]Alilelewa katika familia ya Kisufi yenye msimamo wa kihafidhina nchini Sudan na baadaye alikimbilia Norway kama mkimbizi wa kisiasa mwaka wa 2008 kutokana na mwelekeo wake wa kijinsia.[2]Kazi zake za sanaa zinachanganya utamaduni wa Sudan (kama vile Mafarao Weusi wa Ufalme wa kale wa Kush) na ushawishi wa nchi za Magharibi. Alishirikishwa katika filamu ya maandishi ya mwaka 2020 iitwayo The Art of Sin.[3]
Maisha na Kazi ya Ahmed Umar
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya Awali na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Ahmed Umar alizaliwa Sudan kwa wazazi Siddig na Zeinab Umar, akiwa mdogo kuliko ndugu watano.[4]Alipata elimu yake huko Makka, Saudi Arabia, ambapo alianza kutambua hisia zake kwa wavulana wenzake. Baadaye alirejea Sudan kwa masomo ya juu kabla ya kuhamia Norway.Nchini Norway, alihitimu shahada ya kwanza ya sanaa ya uchapishaji (Printmaking) mwaka 2014 na baadaye shahada ya uzamili (Master’s degree) katika Sanaa Nzuri kutoka Chuo cha Kitaifa cha Sanaa cha Oslo (Oslo National Academy of the Arts).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahmed Umar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ Umar uses he/him, she/her, and they/them pronouns. This article uses he/him for editorial consistency.
- ↑ Jahshan, Elias (2022). "Ahmed Umar: Pilgrimage to Love". This Arab is queer : an anthology by LGBTQ+ Arab writers. pp. 75–82. ISBN 978-0-86356-478-9. OCLC 1334646295
- ↑ Ahmed Umar: On hair, art and queerness". My Kali. 18 August 2022. Archived from the original on 23 October 2022. Retrieved 24 October 2022
- ↑ Melvær, Mia (9 December 2020), "Ahmed Umar", Store norske leksikon (in Norwegian Bokmål), archived from the original on 24 October 2022, retrieved 26 October 2022