Ahmad Qavam
Ahmad Qavam (2 Januari 1873 – 23 Julai 1955), anajulikana pia kama Qavam os-Saltaneh (alikuwa mwanasiasa wa Iran alihudumu kama Waziri Mkuu wa Iran katika vipindi vitano tofauti.
Maisha ya mapema
[hariri | hariri chanzo]Ahmad Qavam alizaliwa mnamo mwaka 1873 katika familia mashuhuri ya Familia ya Mostowfian Ashtiani. Mjomba wake, Amin al-Dowleh, alikuwa Waziri Mkuu wa Iran. Kaka yake mkubwa alikuwa Hasan Vossug, ambaye pia alihudumu kama Waziri Mkuu wa Iran mara mbili.[1] Mapema katika taaluma yake, Qavam alihudumu katika jumba la kifalme la Naser al-Din Shah Qajar na kupata jina la cheo la os-Saltaneh wakati wa Mapinduzi ya Katiba ya Iran mnamo mwaka 1909. Barua iliyotiwa saini na Mozaffar ad-Din Shah Qajar ya kukubali Mapinduzi ya Katiba iliandikwa na Qavam, ambaye wakati huo alikuwa na cheo cha Dabir-e Hozoor (Katibu Binafsi). Qavam alikuja kuwa Waziri Mkuu mara kadhaa katika enzi za Nasaba ya Qajar na Utawala wa Pahlavi. Mara mbili alicheza kura muhimu sana katika kuzuia Umoja wa Kiovyeti usinyakue mikoa ya kaskazini mwa Iran.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ James A. Bill (1988). The Eagle and the Lion. The Tragedy of American-Iranian Relations. New Haven and London: Yale University Press. uk. 108. doi:10.12987/9780300159516-006. ISBN 978-0-300-04412-6.
{{cite book}}: Unknown parameter|s2cip=ignored (help)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahmad Qavam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |