Ahazia wa Yuda
Mandhari

Ahazia wa Yuda (kwa Kiebrania: אֲחַזְיָהוּ, ʼĂḥazyāh; pia: Jehoahaz I; 863 KK hivi - 841 KK hivi) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 842 KK na 841 KK baada ya baba yake Yehoramu.
Alipofariki dunia kwa kuuawa bado kijana, mama yake Atalia, binti Ahabu, aliteka madaraka kwa kuua watoto wa Ahazia na kuendeleza sera za ufalme wa Israeli dhidi ya Mungu pekee, YHWH.
Hata hivyo, Yehosheba, dada wa Ahazia, alifaulu kumuokoa mtoto wake mmoja, Yehoashi, akamlea kwa siri hekaluni akishirikiana na mumewe, kuhani Yehoyada, hata akaweza kumtawaza katika kiti cha enzi cha babu yao Daudi.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 8-9 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 22.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahazia wa Yuda kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |