Agwara (ngoma)
Agwara ni ngoma ya kifalme ya Waalur wa Kaskazini mwa Uganda, inayochezwa mbele ya mfalme wao (Rwot).[1] Ngoma hii huchezwa na wanawake na wanaume wakati wa hafla za kijamii. Hupigwa kwa ala za ngoma, na hufuata mpangilio wa mistari au duara, huku wachezaji wakipinda miguu na viuno kwa ustadi wakiwa wamevaa kengele kwenye vifundo vya miguu ili kusisitiza mienendo ya miguu yao.[2][3] Asili ya ngoma hii ilianza wakati watu wa Alur walipokuwa wakichanganya na kupaka tope kwenye nyumba zao.[4]
Utumbuizaji wa ngoma
[hariri | hariri chanzo]Hapo zamani, Agwara ilikuwa ikichezwa katika matambiko yaliyopangwa na jamii kwa ajili ya kuabudu au kupatanisha miungu. Ngoma hii ilichezwa ili kuomba mavuno mazuri kabla ya kupanda, wakati wa sherehe za katikati ya kiangazi au baridi, au wakati wa kuingia katika awamu mpya ya mwezi, au pale ambapo kulihitajika mvua.
Aidha, kuna aina mbili za Agwara, "Kwaya" au "Mbaka", ambazo huchezwa kwa muda wa siku mbili hasa kwa ajili ya mashindano ya koo, na"Selewa", ambayo huchezwa kwa kawaida kama ishara ya kutoa shukrani.[5][6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Rwot Ubimi urges subjects on developing kingdom". New Vision (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
- ↑ "Cultural Dances in Uganda". Waka Natures (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-27. Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
- ↑ "Alur". 101 Last Tribes. Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
- ↑ Dennis, Oneka (2011-05-06). "Agwara dance". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-09. Iliwekwa mnamo 2025-07-23.
{{cite journal}}: Cite journal requires|journal=(help) - ↑ "Celebrating the wealth of ethnicity". Monitor (kwa Kiingereza). 2021-01-05. Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
- ↑ "Background on the Music of Northern Uganda". Singing Wells (kwa American English). 2012-10-29. Iliwekwa mnamo 2024-01-27.
| Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Agwara (ngoma) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |