Nenda kwa yaliyomo

Agostino Trivulzio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kumbukumbu ya Kardinali Trivulzio, S. Maria del Popolo

Agostino Trivulzio (takriban 14851548) alikuwa askofu, kardinali na mjumbe wa papa kutoka Italia.

Alitoka familia ya kifahari huko Milano, mtoto wa nane wa Giovanni Trivulzio di Borgomanero, mshauri wa watemi wa Milano, na Angela (au Agnolina, au Anna) Martinengo wa Brescia. Hivyo alikuwa na undugu na Kardinali Gianantonio (au Antonio) Trivulzio (1500–1508).[1] Baba mwingine, Teodoro, ndugu wa Kardinali Antonio, alikuwa Gavana wa La Palice, wa Genoa (kuanzia mwaka 1526), wa Milano, na Kamanda wa Ufaransa. Giovanni na Angela walikuwa na binti aitwaye Damigella au Domtilla ambaye alikuwa maarufu kwa elimu yake. Kardinali Agostino Trivulzio alikuwa na mpwa aitwaye Giovanni, ambaye alioa Laura Gonzaga.[2]

  1. Georgio Viviano Buonaccorsi (1751). Antichità ... del Protonotariato Appostolico partecipante (kwa Italian). Faenza: Benedetti. ku. 280–281.{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  2. J. P. Adams, Sede Vacante 1521-1522. Retrieved: 2016-05-14. F. Petruccelli della Gattina, Histoire diplomatique des conclaves Volume I (Paris: 1864), 512-526.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.