Nenda kwa yaliyomo

Agnes Quaye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Agnes Quaye (alizaliwa tarehe 5 Oktoba, 1989) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa wanawake kutoka nchini Ghana anayekipiga kama kiungo wa kati katika timu ya taifa ya wanawake ya Ghana.

Maisha ya awali na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Quaye alizaliwa mwaka 1989. Alikuwa akichezea klabu ya mpira ya Nungua Ladies mjini Accra wakati alipokuwa sehemu ya timu ya taifa mwaka 2007 katika Michezo ya Afrika yote (All Africa Games).[1][2]

Huo ulikuwa mwaka wa pili kwa wachezaji wa soka wa wanawake kualikwa kushiriki michezo hiyo, lakini ulikuwa mara ya kwanza Ghana kujumuishwa. Quaye alikuwa katika kikosi hicho pamoja na Naomi Asante, Mary Niiquaye, Jennifer Opoku, Ama Saabi, Sakina Abdul, Priscilla Annor, Lydia Kwarteng, Evelyn Amaning na Portia Boakye.

  1. "Princesses, Queens Back To Camp". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-22.
  2. Association, Ghana Football. "Princesses stun Liberia in 4-0 win". www.ghanafa.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-22.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Agnes Quaye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.