Nenda kwa yaliyomo

Agnes Chigabatia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Agnes Asangalisa Chigabatia
Amezaliwa 20 Oktoba 1956
Amekufa 9 Januari 2024
Nchi Ghana

Agnes Asangalisa Chigabatia (20 Oktoba 1956 - 9 Januari 2024) alikuwa mwanasiasa kutoka nchini Ghana. Aliwahi kuwa mbunge wa eneo la Builsa North katika bunge la Ghana[1][2].

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Agnes Chigabatia alizaliwa tarehe 20 Oktoba 1956 huko Chuchuliga, wakati huo ikiitwa Gold Coast (kwasasa inafahamika kama Mkoa wa Upper East, Ghana).

Alipata elimu ya shule ya kati katika Shule ya Adda Middle School huko Navrongo na Ayieta Middle School huko Sandema. Baadae aliendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Wasichana ya St. Francis Senior High School, Jirapa.Aliendeleza masomo yake zaidi katika Chuo cha Accra Polytechnic, ambapo alipata cheti cha ngazi ya juu katika masomo ya upishi[3].

Chigabatia alikuwa mtaalamu wa masuala ya upishi.

  1. https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/NewsArchive/Former-MP-condemns-politicians-campaigning-with-akpeteshie-713434
  2. https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/NewsArchive/Hon-Agnes-Chigabatia-For-Vice-President-126166
  3. Sam, Eben C. (2005-01-15). The Mirror: Issue2614 January 15 2005 (kwa Kiingereza). Graphic Communications Group.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Agnes Chigabatia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.