Nenda kwa yaliyomo

Africa Tsoai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Africa Tsoai
Amezaliwa 4 July 1967
Afrika kusini
Kazi yake Mwigizaji, mtengenezaji filamu, mfanyabiashara
Watoto 4

Africa Tsoai (alizaliwa 4 Julai 1967)[1]ni mwigizaji na mfanyabiashara kutoka Afrika Kusini anayejulikana zaidi kwa kuigiza kama Tsokotla katika tamthilia ya runinga Mokgonyana Mmatswale na kama John Maputla katika Skeem

Afrika Tsoai ameigiza katika tamthilia nyingi za zamani, na maarufu zaidi kwa kuigiza katika tamthilia ya miaka ya 80 Mokgonyana Mmatswale kama Tsokotla, kijana aliyekuwa dereva wa teksi na aliyependa mwanamke mzee kuliko yeye. Hata hivyo, umaarufu wake mkubwa unatokana na nafasi yake kama John Maputla, mume wa Meikie Maputla na baba wa Leeto na Thabo Maputla katika tamthilia ya Skeem Saam inayorushwa na SABC 1[2]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Africa Tsoai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Peris Walubengo (2019-09-30). "Africa Tsoai biography: age, children, wife, family, Skeem Saam, and interview - Briefly.co.za". briefly.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-09-27.
  2. "Skeem Saam", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2025-08-20, iliwekwa mnamo 2025-09-27