Nenda kwa yaliyomo

Affaf Tobbala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Affaf Tobbala
AmezaliwaJulai 12, 1941 Cairo
UtaifaMisri
Kazi yakeMtayarishaji na Muandaaji wa Makala za Televisheni

Affaf Tobbala (amezaliwa Kairo, 12 Julai 1941) ni mwongozaji na mtayarishaji wa filamu za makala za televisheni, na pia ni mwandishi wa fasihi za watoto kutoka Misri. Tobbala amewahi kuteuliwa na pia kushinda tuzo kadhaa za kifasihi ndani ya Misri na nje ya nchi.[1] Kitabu chake cha mwaka 2006, Sika and Mokka, kilipata Tuzo ya Suzan Mubarak ya Fasihi ya Watoto mwaka 2007, na kilijumuishwa kwenye Orodha ya Heshima ya International Board on Books for Young People (IBBY) mwaka 2010.[2]

Tobbala alizaliwa katika familia ya tabaka la kati. Aliolewa mwaka 1960 baada ya kumaliza elimu ya sekondari katika shule ya wamisionari wa Kifaransa. Tobbala ana watoto wawili, waliozaliwa mwaka 1962 na 1964. Alipata shahada ya kwanza ya Sanaa katika Fasihi ya Kifaransa mwaka 1965, na shahada ya Uzamili (1987) pamoja na Uzamivu (PhD, 1996) katika mawasiliano ya umma (Mass Communication) kutoka Chuo Kikuu cha Cairo.

Tobbala alifanya kazi katika televisheni ya Misri kama mwongozaji, mwandishi wa skripti, na mtayarishaji kuanzia mwaka 1966 hadi 2001, akibobea katika utayarishaji wa filamu za makala (documentaries). Pia alishika nyadhifa kadhaa za uongozi katika nyanja za mipango na upangaji wa vipindi. Tangu mwaka 1987, Tobbala amekuwa akifundisha kozi za televisheni na utayarishaji wa filamu za makala kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza na wataalamu wachanga wa utangazaji katika shule kadhaa (ikiwemo Chuo Kikuu cha Cairo).

  1. https://web.archive.org/web/20170911025204/http://www.bibliotecasalaborsa.it/ragazzi/bibliografie/20428
  2. https://web.archive.org/web/20170911025311/http://www.annalindhfoundation.org/news/list-101-books-exhibition-announced
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Affaf Tobbala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.