Aerosmith
| Aerosmith | |
|---|---|
| Taarifa za awali | |
| Miaka ya kazi | 1970–sasa |
| Studio | Columbia, Geffen, Capitol |
| Wavuti | aerosmith.com |
Aerosmith ni bendi ya muziki wa rock kutoka nchini Marekani iliyoundwa mjini Boston mnamo mwaka 1970.[1][2][3] Bendi hiyo inaundwa na mwimbaji mkuu Steven Tyler, mpiga besi Tom Hamilton, mpiga ngoma Joey Kramer, pamoja na wapiga gitaa Joe Perry na Brad Whitford. Mtindo wao wa muziki una msingi kwenye blues na hard rock,[4][5] pia ukiingiza vipengele vya pop rock,[6] heavy metal,[4] glam metal,[7] na rhythm and blues,[8] na umevutia wasanii wengi wa baadaye wa rock.[9] Mara kadhaa Aerosmith inajulikana kama "The Bad Boys from Boston"[10] na "America's Greatest Rock and Roll Band".[11][12][13] Timu kuu ya uandishi wa nyimbo ya Tyler na Perry mara zote hupewa jina la "Toxic Twins".
Perry na Hamilton mwanzoni walikuwa pamoja kwenye bendi iliyoitwa Jam Band, ambapo walikutana na Tyler, Kramer, mpiga gitaa Ray Tabano, na kuunda Aerosmith; mnamo 1971, Tabano alibadilishwa na Whitford. Walitoa mfululizo wa albamu zilizopata mafanikio makubwa kuanzia albamu yao ya kwanza iliyoitwa kwa jina lao wenyewe Aerosmith mnamo 1973, ikifuatiwa na Get Your Wings mwaka mmoja baadaye.[14] Bendi hiyo ilipata umaarufu mkubwa kupitia albamu mbili zilizofuata, Toys in the Attic (1975) na Rocks (1976).[15] Albamu za Draw the Line na Night in the Ruts zilifuata mnamo 1977 na 1979. Katika miaka ya 1970, bendi hiyo ilifanya ziara nyingi na kuingiza nyimbo kadhaa kwenye chati za Billboard Hot 100, ikiwa ni pamoja na wimbo wao wa kwanza kufika Top 40, "Sweet Emotion", pamoja na nyimbo zilizofika Top 10 kama "Dream On" na "Walk This Way". Kufikia mwishoni mwa muongo huo, walikuwa miongoni mwa bendi maarufu zaidi za hard rock duniani na kuwa na mashabiki wengi waliojulikana kama "Blue Army".[16] Matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya na migogoro ya ndani yalisababisha kuondoka kwa Perry na Whitford mnamo 1979 na 1981.[5] Bendi hiyo haikufanya vyema na albamu ya Rock in a Hard Place (1982) haikufikia mafanikio ya hapo awali.
Perry na Whitford walirejea Aerosmith mnamo 1984. Baada ya ziara ya kurejea, walirekodi Done with Mirrors (1985), ambayo haikufikia matarajio ya kibiashara. Haikuwa hadi waliposhirikiana mnamo 1986 na kundi la rap la Run–D.M.C. kurudia wimbo wa "Walk This Way", pamoja na albamu yao iliyouza sana ya Permanent Vacation (1987), ndipo waliporejesha kiwango chao cha zamani cha umaarufu.[17] Mwishoni mwa miaka ya 1980 na 1990, bendi ilishinda tuzo nyingi kupitia albamu za Pump (1989), Get a Grip (1993), na Nine Lives (1997). Nyimbo zao maarufu zaidi katika kipindi hiki ni pamoja na "Dude (Looks Like a Lady)", "Angel", "Rag Doll", "Love in an Elevator", "Janie's Got a Gun", "What it Takes", "Livin' on the Edge", "Cryin'", na "Crazy". Pia walitengeneza video maarufu za muziki na kuonekana kwenye televisheni, filamu na michezo ya video. Mnamo 1998, walipata wimbo wao wa kwanza kushika nafasi ya kwanza kupitia "I Don't Want to Miss a Thing" kutoka kwenye albamu ya filamu ya Armageddon. Kurejea kwao kuemelezewa kama miongoni mwa mambo ya kuvutia zaidi katika historia ya rock.[4][5] Albamu zingine kama Just Push Play (iliyojumuisha wimbo wa "Jaded"), Honkin' on Bobo, na Music from Another Dimension! zilifuata mnamo 2001, 2004, na 2012. Baada ya Steven Tyler kuumia sauti mnamo 2023, Aerosmith walitangaza kustaafu kufanya ziara za matamasha mnamo 2024. Walitoa muziki wao mpya wa kwanza baada ya miaka kumi na tatu kupitia EP ya ushirikiano na Yungblud, One More Time, mnamo 2025.
Aerosmith ndiyo bendi ya Marekani ya hard rock iliyouza rekodi nyingi zaidi katika historia, ikiwa imeuza zaidi ya nakala milioni 150 duniani kote.[18][19] Wameshinda tuzo nne za Grammy, tuzo sita za American Music Awards, na tuzo kumi za MTV Video Music Awards. Waluingizwa kwenye Ukumbi wa Sifa wa Rock and Roll (Rock and Roll Hall of Fame) mnamo mwaka 2001,[20] na mnamo 2013, Tyler na Perry walioingizwa kwenye Ukumbi wa Sifa wa Waandishi wa Nyimbo (Songwriters Hall of Fame).
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu za Studio
- Aerosmith (1973)
- Get Your Wings (1974)
- Toys in the Attic (1975)
- Rocks (1976)
- Draw the Line (1977)
- Night in the Ruts (1979)
- Rock in a Hard Place (1982)
- Done with Mirrors (1985)
- Permanent Vacation (1987)
- Pump (1989)
- Get a Grip (1993)
- Nine Lives (1997)
- Just Push Play (2001)
- Honkin' on Bobo (2004)
- Music from Another Dimension! (2012)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Aerosmith | The Rock and Roll Hall of Fame and Museum". Rockhall.com. Aprili 15, 2013. Iliwekwa mnamo Agosti 26, 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Burlingame, Jeff (2018-12-15). Aerosmith (kwa Kiingereza). Enslow Publishing, LLC. uk. 29. ISBN 978-1-9785-0521-6.
- ↑ Furniss, Matters (Februari 2012). Aerosmith - Uncensored on the Record (kwa Kiingereza). Coda Books Ltd. ISBN 978-1-78158-014-1.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 Stephen Thomas Erlewine. "Aerosmith Biography". Allmusic. Iliwekwa mnamo Agosti 22, 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 "Aerosmith: Biography: Rolling Stone". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 30, 2015. Iliwekwa mnamo Agosti 22, 2016.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Cater, Darryl. "Aerosmith & KISS will be performing at the Tweeter Center on September 26, 2003". ChicagoGigs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 28, 2007. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2008.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Pareles, Jon (Julai 10, 1988). "Heavy Metal, Weighty Words – NYTimes.com". The New York Times. Iliwekwa mnamo Mei 16, 2010.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Coleman, Mark. "Aerosmith: Get A Grip: Music Reviews: Rolling Stone". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 5, 2008. Iliwekwa mnamo Machi 31, 2008.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "allmusic – Pop-Metal". AllMusic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 5, 2012. Iliwekwa mnamo Aprili 12, 2008.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Aerosmith Biography". The Rock and Roll Hall of Fame and Museum. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 19, 2012. Iliwekwa mnamo Oktoba 20, 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Newman, Melinda (Agosti 15, 1998). "The Billboard Interview – Aerosmith". Billboard. Juz. 110, na. 33. ku. 19–20. ISSN 0006-2510.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ives, Brian. "Aerosmith's Opening Night: Crazy Amazing For Hell's Angels And 'Jaded' Kids". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 28, 2010.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mieses, Stanley (Agosti 9, 1997), "Still Walking the Walk, Leading the Way", Newsday, uk. B.05
{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Murrells, Joseph (1978). The Book of Golden Discs (tol. la 2nd). London: Barrie and Jenkins Ltd. uk. 341. ISBN 0-214-20512-6.
- ↑ "Aerosmith Just Keeps on Rockin'". Articlecity.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 7, 2011. Iliwekwa mnamo Aprili 6, 2008.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Davis, p. 239
- ↑ "Aerosmith – Full Biography". The New York Times. 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 4, 2015. Iliwekwa mnamo Aprili 18, 2019.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ DiGiacomo, Robert (Agosti 27, 2014). "Aerosmith guitarist Perry tells all; band hits A.C. Sunday". The Press of Atlantic City. Iliwekwa mnamo Oktoba 15, 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Top Selling Artists". Recording Industry Association of America (RIAA.com). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 1, 2007.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The Immortals – The Greatest Artists of All Time: 57) Aerosmith". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 1, 2008. Iliwekwa mnamo Machi 25, 2008.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)