Adrian Atiman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Adrian Atiman (Tindirma, Sudan ya Kifaransa, leo Mali, 1866 hivi [1] - Karema, mkoa wa Katavi, 24 Aprili 1956[2]) alikuwa katekista na daktari wa Kiafrika mmisionari nchini Tanzania[3].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Msonghai, alikombolewa na Wamisionari wa Afrika kutoka utumwa huko Metlili, kusini mwa Algeria[4].

Baada ya kusomeshwa hadi Ulaya[1] aliishi na kufanya kazi katika misheni ya Karema kuanzia mwaka 1889[5] hadi kifo chake akiheshimiwa na wote[2] kwa huduma zake zilizomfikisha hata vijiji vya mbali[2].

Aliacha mke na mtoto mmoja, padri Joseph[5], pamoja na masimulizi ya maisha yake.[6]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Dr. Adrien Atiman". The British Medical Journal 1 (4978): 1305. 2 June 1956.
  2. 2.0 2.1 2.2 J. Grosjean, Atiman (Adrien), Biographie Belge d'Outre-Mer, vol. 7-C (1989), 12-16.
  3. Atiman, Adrian.
  4. Rockel, Stephen (16 April 2013). "The Remarkable Story of Adrian Atiman: Freed Slave to Medical Missionary" (in en). SSRN.
  5. 5.0 5.1 Atiman, Adrien.
  6. African history specialist discusses Adrien Atiman, freed slave to medical missionary. York University. Iliwekwa mnamo 18 August 2020.

Marejeo kwa Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

  • George Pelz, "Katekista na daktari Adrian Atiman"
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.