Nenda kwa yaliyomo

Adenike Grange

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Adenike Grange ni profesa wa watoto, mshauri, mwandishi na Waziri wa zamani wa Afya wa kutoka nchi ya Nigeria. Alichaguliwa mnamo 25 Julai 2007, na kufanikiwa kuwa Waziri wa kwanza wa Afya mwanamke ndani ya nchi ya Nigeria. Kipindi cha utawala wake, alifanya kazi kwa lengo la kuweka vizuri zaidi utoaji wa huduma za afya, kupunguza vifo vya akina mama na magonjwa miongoni mwa makundi yaliyo hatarini. Alikamatwa kwa amri ya Rais Umaru Musa Yar'Adua kuhusu kushughulikia ₦ milioni 300 za fedha za serikali ambazo hazikutumika. Alichunguzwa na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha (EFCC) na akashtakiwa. Alijiuzulu ofisini tarehe 26 Machi 2008.

Mandharinyuma

[hariri | hariri chanzo]

Grange alipata elimu yake kwenye shule ya sekondari huko Lagos na baada ya hapo kwenye Chuo cha St. Francis, Letchworth ndani ya nchi ya Uingereza . Kwenye mwaka 1958 hadi mwaka 1964 alisomea udaktari ndani ya Chuo Kikuu cha St Andrews huko nchi ya Uskoti. Alifanya kazi ndani ya Hospitali ya Dudley Road huko Birmingham kabla ya kurejea Nigeria mwaka wa 1965, ambapo aliendelea kufanya kazi kwenye hospitali za Lagos. Alihamisha makazi tena Uingereza mwaka wa 1967 na kufanyika kuwa afisa mkuu wa nyumba (watoto) kwenye Hospitali ya Watoto ya St Mary, na akapata Stashahada ya Afya ya Mtoto mwaka wa 1969. Mwaka wa 1971, alijiunga na Hospitali ya Ufundishaji ya Chuo Kikuu cha Lagos . Mwaka wa 1978, akawa mhadhiri kwenye Chuo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Lagos . Akawa mhadhiri mkuu mwaka wa 1981 na profesa mwaka wa 1995. [1]

Grange alihudumu kama mshauri kwa Federal Ministry of Health, WHO, UNICEF, UNFPA and USAID.[2] Yeye anafahamika kama mshauri wa WHO kwa ajili ya maswala ya Programu ya Afya ya Uzazi mwaka 1993 hadi mwaka 1999. Yeye ni mwandishi wa zaidi ya karatasi 50 za kisayansi sana sana juu ya kuhara na mazigira ya lishe kwa watoto. Amehudumu kama raisi wa International Pediatric Association.[3] Kweye kazi yake amefahamika kama mtetezi kwa kuboresha afya ya watoto.[4]

Waziri wa Afya

[hariri | hariri chanzo]

Kwenye mwaka wa 25 Julai 2007, Grange alichaguiwa kuwa Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Shirikisho ya nchini Nigeria, na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Kwenye tarehe 9 Novemba 2007, Grange alisoma Hotuba ya Lancet kwenye Kituo cha Afya na Maendeleo ya Kimataifa cha UCL .

Alielezea, "Kuna utoshelevu juu ya suala la mipango ya maarifa, mikakati, zana, dawa na itifaki za matibabu ili kutibu magonjwa na kuongeza muda wa kuishi, japo ukweli ni kwamba mifumo iliyoundwa ili kuleta matokeo haya haijitoshelezi au hamna kabisa, swala ambalo ni changamoto kwa mataifa". Alisema kufanya kazi nchi ya Nigeria ili kuweka sawa mbinu za utoaji wa huduma za afya na kuiga mbinu bora kutoka nchi zingine. Vipaumbele viliunganisha kutokomeza polio, kudhibiti malaria, kupunguza vifo vya akina mama, na kupunguza viwango vya magonjwa katika makundi yaliyo hatarini zaidi. [5]

Kwenye mwaka Januari 2008, ndani ya hafla iliyohudhuriwa na mke wa rais Turai Umar Musa Yar'Adua, Grange alimwomba mke wa rais kuweka umakini wa kitaifa kwa umuhimu wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayo husu swala la afya. Alitoa wito kwa Bunge la Kitaifa kupitisha kwa haraka kwa muswada wa afya wa kitaifa, na aliwataka wake wa magavana wa majimbo kuweka nguvu juu ya sheria za kukuza ustawi wa wanawake na watoto. [6]

  1. ↑ "Professor Adenike Grange" (PDF). World Health Organization. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ Pediatrics, American Academy of (2007-09-01). "Dr. Grange named Nigerian health minister". AAP News (kwa Kiingereza). 28 (9): 40. ISSN 1073-0397.
  3. ↑ "Welcoming Adenike Grange and Gabriel Aduku". Nigeria Health Watch. 27 Julai 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Aprili 2010. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ "Article: Adenike Grange – Crusading for the African Child's Health". Women & Environments International Magazine Article. 1 Oktoba 2002. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-16. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. ↑ "UCL Lancet Lecture: health reform in Nigeria". University College London. 12 Novemba 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-22. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. ↑ Constance Ndubuisi-Enyali (29 Januari 2008). "Turai Yar 'Adua commits to saving women and children". Development Communications Network. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)