Nenda kwa yaliyomo

Adejoke Ayoola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Adejoke Ayoola (alizaliwa 20 Julai 1970) ni mwanamke mwenye utaalamu wa utafiti pamoja na kuwa muuguzi kutoka nchi ya Nigeria ndani ya bara la Afrika mwenye asili ya Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Calvin . [1]

Adejoke alipata masomo yake ya chuo kweney Chuo Kikuu cha Obafemi Awolowo eneo la Ile-Ife, Nigeria, akihitimu shahada za BSN na MSN mwaka wa 1991 na mwaka wa 1998 kwa mtiririko huwo. Alihamisha makazi a Marekani mwaka wa 2001 ili kupanua elimu yake,huku akijipatia elimu ya Shahada ya Uzamivu (PhD) dani ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan, East Lansing, Michigan, mwaka wa 2007.

Adejoke alishika nafasi ya Muuguzi Msomi wa Kitivo cha Robert Wood Johnson Foundation kwenye sekta ya Uuguzi ya Chuo cha Calvin (CCDON) eneo la Grand Rapids, Michigan. [2] [3]

Utafiti wa uuguzi

[hariri | hariri chanzo]

Kazi za Adejoke na wanawake wenza wenye uchumi wa chini waliotokea asili mbalimbali za kikabila kwenye eneo Grand Rapids zilichapishwa kwenye Jarida la Ukunga na Afya ya Wanawake kwenye tarehe Julai 2013. Jumla ya hayo alikuwa mwenye michango mengi kuloko wote kwenye mchakato wa utafiti uliochapishwa kwenye Jarida la Marekani la Obstetrics and Gynecology mwaka wa 2009 ukielezea uhusiano kati ya wakati wa utambuzi wa ujauzito na matokeo ya kuzaliwa, kama vile kuzaliwa kabla ya wakati, uzito mdogo wa kuzaliwa, kulazwa katika kitengo cha utunzaji mkubwa wa watoto wachanga, na vifo vya watoto wachanga. Utafiti wake unajikita juu ya kukuza afya ya uzazi ya wanawake na vijana kwa lengo kuu la kupunguza matokeo duni ya afya ya mama na mtoto. Utafiti wake juu ya vipengele vya maarifa ya afya ya uzazi na upangaji wa ujauzito juu ya jamii tatu za makazi, zenye kipato cha chini zenye makabila tofauti ulikuwa vitongoji vilivyoshirikiana na mpango wa CCDON. Kusudi la mradi huo lilikuwa kupunguza changamoto ya mimba isiyopangwa na kupanua utambuzi wa mapema wa ujauzito. Utafiti wake unaonyesha umuhimu wa utafiti wa uuguzi na umuhimu wa kizazi cha utafiti katika kudumisha utendaji mzuri wa uuguzi, haswa ndani ya mfumo wa huduma ya afya ya Marekani unaobadilika kila mara. Adejoke ni mwanachama wa Jumuiya ya Utafiti wa Wauguzi ya Midwest (MNRS) na Makamu wa Rais wa CCDON wa Jumuiya ya Kimataifa ya Heshima ya Wauguzi ya Sigma Theta Tau, Kappa Epsilon-at-Large. [4] [5] [6] [7]

Nafasi za kitaaluma na heshima

[hariri | hariri chanzo]
  • Mwanachama wa Chuo cha Uuguzi cha Marekani (2020–sasa) [8]
  • Profesa Msaidizi, Agosti 2007–sasa: Idara ya Uuguzi, Chuo cha Calvin, Grand Rapids
  • Msaidizi wa utafiti, Januari 2005–sasa: Idara ya Tiba, Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan .
  • Mwalimu mkuu wa muuguzi, Novemba 2000–Agosti 2003: Shule ya Uuguzi ya Baada ya Msingi, Kituo cha Kitaifa cha Huduma ya Masikio, Lagos, Nigeria.
  • Afisa wa Programu, Septemba 1999–Oktoba 2000: Action Health Incorporated, Lagos, Nigeria
  • Afisa wa programu, Juni 1998–Agosti 1999: Mradi wa Kukuza Afya ya Wanawake, Ile-Ife, Nigeria
  • Mkufunzi wa muuguzi aliyehitimu, Aprili 1994–Juni 1998: Idara ya Uuguzi, Chuo Kikuu cha Obafemi Awolowo, Ile-Ife, Jimbo la Osun, Nigeria
  • Mkufunzi wa mkunga, Mei 1993–Januari 1994: Shule ya Ukunga, Hospitali ya Kikatoliki ya Oluyoro, Ibadan, Jimbo la Oyo, Nigeria.

Machapisho yaliyochaguliwa

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Grand Rapids Magazine". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 17, 2015. Iliwekwa mnamo Aprili 17, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Brian McVicar (Agosti 29, 2012). "Calvin College nursing professor wins $350,000 to educate low-income women about unplanned pregnancy". Mlive Media. Iliwekwa mnamo Aprili 17, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Ayoola Adejoke". Nursefacultyscholars. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 17, 2015. Iliwekwa mnamo Aprili 17, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Ayoola, Adejoke (8 Aprili 2017). "Preconception Reproductive Knowledge Promotion (PREKNOP)". {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Top Professors and Administrators". CNA. Iliwekwa mnamo Aprili 17, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Congress Program" (PDF). 25th International Nursing Research Program. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo Aprili 17, 2015. Iliwekwa mnamo Aprili 17, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Ayoola, Adejoke B.; Stommel, Manfred; Nettleman, Mary D. (Agosti 2009). "Adejoke Ayoola". 201 (2): 156.e1–156.e6. doi:10.1016/j.ajog.2009.05.011. PMID 19646566. Iliwekwa mnamo Aprili 17, 2015. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Danielle Nelson (4 Novemba 2020). "Calvin nursing professor inducted into American Academy of Nursing". Grand Rapids Business Journal. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Ayoola Adejoke". Office for Research and scholarship, Department of Nursing Calvin College. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-24. Iliwekwa mnamo 2026-04-13.
  • "Adejoke Ayoola". Calvin University.