Abula (supu)
Mandhari
Àbùlà ni chakula kinachotokea kwenye jamii ya Wayoruba kutoka Nigeria. Chakula hiki hujumuisha amala (chakula cha viazi/viazi vikavu vilivyopondwa), ewedu (supu ya majani ya jute yenye ute), gbegiri (supu ya maharagwe) na obe ata (mchuzi wa nyanya wenye pilipili).[1][2]
Àbùlà huchukuliwa kama chakula maalum (delicacy) kwa sababu si chakula cha kawaida na huhitaji muda na juhudi nyingi kukiandaa. Mara nyingi huliwa na watu wa Kiyoruba, hasa katika maeneo ya Ọ̀yọ́ na Ogbómòṣọ́.[3]
Viambato
[hariri | hariri chanzo]Gbegiri (supu ya maharagwe):
- Maharagwe
- Maji
- Vitunguu (hiari)
- Pilipili iliyosagwa (ata rodo / pilipili kali) (hiari)
- Mafuta ya mawese
- Viungo na chumvi
- Majivu ya potashi (potash)
Ewedu (supu ya majani ya jute):
- Majani ya ewedu
- Mbegu za locust (iru/dawadawa)
- Potashi
- Chumvi
- Maji
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Abula (soup)", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-03-20, iliwekwa mnamo 2026-04-06
- ↑ The Nation (2017-10-20). "Best Nigerian recipe for this weekend - Abula". The Nation Newspaper (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-06.
- ↑ Our Reporter (2018-08-29). "Ogbomoso Ajilete group celebrates Amala, Gbegiri Day". Tribune Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-06.