Nenda kwa yaliyomo

Abigail Marshall Katung

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Abigail Wok Marshall Katung (alizaliwa 7 Desemba 1975) ni mwanasiasa wa Nigeria na mke wa seneta anayewakilisha Kaduna State, Nigeria, Sunday Marshall Katung. Alizaliwa na kukulia Nigeria, lakini alihamia Uingereza kusoma katika Chuo Kikuu cha Leeds na ilipofika Januari 2024 akawa mkuu katika chuo kikuu cha Leeds City College. Mnamo Mei 2024, alichukua nafasi ya Lord Mayor wa chuo kikuu cha Leeds,[1] akawa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kushika nafasi hiyo katika baraza la jiji,[2] mtu wa pili mweusi baada ya Eileen Taylor na wa 130 kwa ujumla.[3]

Mnamo mwaka 2008, alianzisha shirika la David Oluwale Memorial Association (DOMA) kwa ajili ya kumuenzi David Oluwale,[4] mhamiaji kutoka Nigeria aliyeingia jijini Leeds mnamo mwaka 1949. Hata hivyo, mwaka 1969, Oluwale alizama katika Mto Aire, na maafisa wawili wa polisi wa Uingereza walihusishwa moja kwa moja na kifo chake. Mnamo Novemba 1971, kesi dhidi ya maafisa hao ilifikishwa mahakamani, na ikawa ni mara ya kwanza na ya kipekee hadi sasa ambapo maafisa wa serikali walihukumiwa kwa kifo cha mtu mweusi nchini Uingereza.[5] Aidha, yeye ni mwenyekiti mwenza wa shirika la DOMA (David Oluwale Memorial Association). [4]

Mnamo Mei 2019, baada ya uchaguzi wa Baraza la Jiji la Leeds, Katung alichaguliwa kuwa mwakilishi wa eneo la Little London na Woodhouse. [6]

Manmo mwaka 2020, alikuwa mwanachama waandamizi katika mtandao wa BAME na pia mshindi wa tuzo ya mtandao bora wa wafanyakazi wa BAME katika Jiji la Leeds. [7]

Mnamo mwaka 2022, alihudumu kama mwenyekiti mwenza wa mpango wa Food Champion wa Baraza la Jiji la Leeds, kwa kushirikiana na Gareth Batty MBE FRSA, Mkurugenzi Mtendaji wa FareShare Yorkshire. [8] Vilevile, alihudhuria kama mgeni maalum katika hafla ya Tuzo za Kumbukumbu ya Jordan Sinnott iliyofanyika St. Mary’s, Meston. [9]

Baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza, aligombea tena na kuchaguliwa kwa mara ya pili katika uchaguzi wa eneo la Little London na Woodhouse mwezi Mei 2023. [10]

Mnamo Januari 2024, aliteuliwa kuwa Meya Mkuu (Lord Mayor) wa Jiji la Leeds chini ya Chama cha Labour na Co-operative, akichukua nafasi ya Al Garthwaite. [1] Uchaguzi wake ni kwa muhula wa mwaka 2024/2025. [11]

Katung pia anatajwa kuwa Mwafrika wa kwanza kuwahi kuchaguliwa kuwa Meya katika Baraza la Jiji la Leeds. [2]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Katung ameolewa na Sunday Marshall Katung, ambaye ni wakili na mwanasiasa kutoka Nigeria. Kufikia mwaka 2023, wanandoa hao walikuwa na wana wa mapacha wenye umri wa miaka 19, ambao aliamua kuwalea jijini Leeds. [1]

  1. 1 2 3 Coyle, Hayle (18 Januari 2024). "New Lord Mayor of Leeds takes up role with 'great pride'". BBC News. Leeds. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  2. 1 2 Alkali, Hamza (18 Januari 2024). Aliyu, Ibrahim; Bakare, Adeniyi (whr.). "Dabiri-Erewa hails appointment of Abigail as Lord mayor of Leeds". Radio Nigeria. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-18. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  3. Connolly, James (19 Januari 2024). "Abigail Marshall-Katung 'honoured and humbled' to become Leeds' first African Lord Mayor". Yorkshire Evening Post. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2024.
  4. 1 2 Gee, Baba (8 Novemba 2023). "The Hibiscus Rising Gala Dinner: A Night of Remembrance and Optimism". African Voice. Leeds. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  5. Athwal, Harmit (18 Oktoba 2010). "The racism that kills". The Guardian. London. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  6. Akhaine, Saxone (5 Mei 2019). "Nigerian woman, Katung wins Leeds City Council election". The Guardian Nigeria. Kaduna. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  7. "Latest key messages from the CLT and BAME network steering group". Leeds City Council. 18 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  8. "Leeds City Council asks public to feedback on first citywide food strategy". Leeds Star. Leeds. 21 Oktoba 2022. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  9. Lomax, Claire (22 Desemba 2022). "Jordan Sinnott Awards inspire young people home and away". Wharfedale Observer. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2024.
  10. Hassan-Wuyo, Ibrahim (6 Mei 2023). "Nigerian woman, Katung re-elected in UK Council election". Vanguard Nigeria. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.
  11. Dada, Adekunle (18 Januari 2024). "Jubilation as Nigerian Woman Elected Lord Mayor of Leeds in United Kingdom". Legit.ng. Iliwekwa mnamo 18 Januari 2024.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]