Abdul Sheriff

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sheriff.

Abdul Sheriff ni profesa mstaafu wa historia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyekuwa pia mkurugenzi wa Beit el Amani (Jumba la kumbukumbu) ambayo ni makumbusho ya kitaifa ya Zanzibar.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Sheriff alizaliwa mnamo 7 Desemba 1939 kwenye kisiwa cha Unguja.

Alipata nafasi ya kusoma Marekani kwa msaada wa masomo ya African Scholarship Program ya Vyuo Vikuu vya Marekani. Alihitimu shahada ya kwanza katika jiografia mnamo 1964 kwenye Chuo Kikuu cha Kalifornia, Los Angeles, na pia shahada ya uzamili katika historia mnamo 1966. Kwenye Chuo cha Masomo ya Mashariki na Afrika huko London alihitimu uzamivu mnamo 1971 kwa msingi wa utafiti wake juu ya historia ya Afrika.

Tangu mwaka 1969 alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kuanzia 1977 hadi 1979 aliongoza kitivo cha historia kama profesa mshiriki akaongoza Shirika la Historia la Tanzania. Mnamo 1980, alikuwa profesa katika chuo kikuu hadi 1996. Isitoshe, alikuwa profesa mgeni katika vyuo vikuu huko Berlin, Lisbon, Bergen, Montreal na Minnesota.

Katika kazi yake ya kitaalamu Sheriff alichunguza utamaduni wa majahazi ya Bahari ya Hindi, historia na utamaduni wa Zanzibar, na historia pamoja na utunzaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar. Ametumia maarifa yake katika ukarabati wa jumba la mapokezi la Sultani akafundisha wasimamizi wa kazi hiyo. Alifaulu kufikia tangazo la Nyumba ya Maajabu kama jumba la kumbukumbu la kitaifa na kitamaduni la Zanzibar.

Mnamo 2005 na 2006 Sheriff alipokea tuzo za kuheshimu michango yake katika uhifadhi wa urithi wa kitamaduni wa Zanzibar.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

  • 1987: Viungo vya watumwa & Ivory Zanzibar: Ushirikiano wa Biashara ya Afrika Mashariki, Vyombo vya Habari vya Chuo Kikuu cha Ohio,
  • 1991: Zanzibar Chini ya Utawala wa Kikoloni: Mafunzo ya Afrika Mashariki, alikutana na Ed Ferguson, Chuo Kikuu cha Waandishi wa Habari cha Ohio,  
  • 1995: Historia ya Zanzibar, ulikutana na Javed Jafferji & Ashter Chomoko, Machapisho ya Hsp,  
  • 1995: Makomandoo wa Zanzibari la Unguja ya Zamani ya Zanzibar, Machapisho ya HSP,  
  • 1995: Historia ya Zanzibar: Upendo wa Zama, Machapisho ya HSP,  
  • 1995: Historia na Uhifadhi wa Jiji la Jiwe la Zanzibar, Vyombo vya Habari vya Chuo Kikuu cha Ohio,  
  • 1998: Mji wa jiwe la zambarau  : utafutaji wa usanifu, alikutana na Zarina Jafferji, Machapisho ya Matunzio, ASIN B007ERZZVG
  • 2001: Jiwe la Jiwe la Zanzibar, ulikutana na Zarina Jafferji, Machapisho ya Galley,  
  • 2006: Jumba la kumbukumbu ya Jumba la Maajabu la Zanzibar: Kujitegemea na Ushirikiano, Utafiti wa Uchunguzi katika Utamaduni na Maendeleo, ulikutana na Paul Klooft & Mubiana Luhila, Wachapishaji wa KIT Amsterdam,  
  • 2010: Tamaduni za Dhow na Bahari ya Hindi: cosmopolitanism, Commerce, and Islam, KIT Publishers Amsterdam,  

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]