Abbah Process

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Abbah Process
Jina la kuzaliwa Sweetbert charless mwinula
Pia anajulikana kama Abbah Process,The hit monster
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Hiphop, Bongo_Fleva,R&B
Kazi yake Mwanamuziki na Muandaaji wa Muziki
Ala R&B
Miaka ya kazi 15
Studio Abbah Music
Ame/Wameshirikiana na Harmonize, Mauasama, Darassa, Sho Madjozi, Richmavoko
Tovuti https://abbah-music.com
Ala maarufu
R&B
ABBAH Proces

Sweetbert Charles mwinula (Abbah process) (amezaliwa 28 July 1994) ni mwanamuziki na muandaaji wa muziki nchini Tanzania. [1][2] Alijizolea umaarufu mwingi kupitia kazi zake ambazo aliziandaa na ambazo ameshirikishwa na alizofanya yeye mwenyewe, Mfano "Maisha na Muziki" Ya Darassa[3], "Chibonge" ya Marioo, Bytarbeast na Abbah. Hizo ni baaadhi ya kazi ambazo alizifanya zikampatia umaarufu mkubwa Barani Afrika na nje yake na kupelekea kushindanishwa kwenye vinyang'anyiro mbalimbali Africa. [4]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Abbah alizaliwa mkoa wa Dar es Salaam hospitali ya Amana, na tangu akiwa mdogo alipendelea kupiga ala za muziki. Baada ya kumaliza masomo yake akajikita rasmi kwenye tasnia ya muziki, na mwaka 2015 alifanikiwa kumiliki stuo yake mwenyewe. Hapo aliweza kuwasaidia vijana wengi wa Kitanzania kufikia malengo yao, kwa kuchukua vijana wenye vipaji vichanga na kuviendeleza zaidi. Alimsaidia Marioo, Bytar [5], Kapipo na the MixKiller. [6]

Abbah alifanikiwa kujizolea umaarufu katika nchi za jirani na Tanzania ambazo ni Kenya na Uganda. [7]

Abbah Music[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2019 Abbah alifungua kampuni ya Muziki, yenye makazi yake Jijini Dar es salaam, kampuni hiyo ambayo inajikita kwenye maswala ya uandaaji wa Muziki, usimamizi wa kazi za wasanii, usimamizi wa wasanii, Kituo cha kufundisha uandaaji muziki. ambapo kupitia kampuni hiyo na Vijana aliowafunza waliweza kutoa mchango mkubwa kwenye albam ya Muziki ya msanii Kubwa Africa na ikiwa imewashirikisha wasabi nguli kutoka Africa, kama Burna Boy, Morgan Heritage, Yemi Alade na wengine wengi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Abbah Lyrics, Biography and Videos | Afrika Lyrics. afrikalyrics.com. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  2. "Music of Tanzania", Wikipedia (in English), 2020-04-13, retrieved 2020-05-11 
  3. ONE ON ONE: Darassa (en). Daily Nation. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  4. Victor Kileo TZA. List kamili ya washindi wa tuzo za Sound City MVP 2020 – Millardayo.com (en-US). millardayo.com. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  5. TDBN- TANZANIA (2020-04-07). Producer Abbah amtambulisha msanii mpya Bytar, afananishwa na Burna Boy (Video) (en-US). World's Breaking News Journal | TDBN |. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  6. Producer Abbah amtambulisha msanii mpya Bytar, afananishwa na Burna Boy (Video) (en-US). Bongo5.com (2020-04-07). Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  7. 707 AND THE GREAT GATSBY EVENT.., – Nuru The Light. blog.nuruthelite.com. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abbah Process kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.