Mazingira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 19:43, 19 Julai 2020 na Idd ninga (majadiliano | michango) (#WPWP #WPWPTZ)
Mazingira ya kiafrika

Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka kiumbe katika maisha yake. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako.

Mazingira huweza kuundwa na vitu mbalimbali; yanaweza kuwa ya asili (kama misitu, milima, maziwa, mabonde, mito, bahari n.k.) au ya kutengenezwa na binadamu (kama majengo, viwanda n.k.).

Hivyo tunapaswa tuwe makini katika kujenga mazingira yetu kwa sababu vitu vingine huyaharibu, kama vile uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa bahari, uchafuzi wa ardhi, n.k.

Tunapaswa kutunza mazingira yetu kwa sababu kilimo, ufugaji mvua, n.k. huathiriwa na uchafuzi wa mazingira. Mazingira hutunzwa kwa njia mbalimbali kama vile kupanda miti kwa wingi, kutunza vyanzo vyetu vya maji, na kutumia maji vizuri, hasa katika shughuli za kilimo, ili kuliepuka tatizo la ukame.

Kanuni kuhusu ulinzi wa mazingira

Nchi mbalimbali zina kanuni za ulinzi wa mazingira. Kwa mfano katika nchi ya Marekani, kuna kanuni kuhusu ulinzi wa wanyama wanaokaribia kutoweka. Kanuni hii iko katika sheria ya Endangered Species Act (ESA) iliyopitishwa na rais Richard Nixon mwaka 1973. Pia kuna mkataba wa kimataifa uitwao Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Flora and Fauna (CITES). Barani Afrika, ulinzi wa mazingira waendeshwa pia japo kuna majangili wanapenda sana kukiuka sheria ili wajitajirishe kwa kuwinda wanyama kiharamu.

Kurasa kuhusu neno mazingira

Mazingira yanaweza kuhusu:

Katika sayansi ya kompyuta:

Viungo vya nje

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: