Kilomita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ufafanuzi wa awali wa kilomita

Kilomita (pia: kilometa) ni kipimo cha urefu. Kinamaanisha urefu wa mita 1,000. Kifupi chake ni km.

Kilomita ni kipimo cha kawaida katika maisha ya kila siku cha kupimia umbali usio karibu. Umbali kati ya miji hupimwa kwa kilomita.

Kilomita ni sehemu ya vipimo vya SI vyenye msingi wa mita.

Katika nchi mbalimbali kilomita imechukua nafasi ya vipimo vingine kama maili au verst.

Kwa umbali mkubwa mno kama kwa vipimo vya astronomia kilomita haifai tena. Hapo kuna vipimo vingine. Kwa mfano umbali kati ya mwezi na dunia inaweza kutajwa kwa kilomita ni lakhi tatu au 300,000 km. Lakini umbali kutoka jua letu hadi nyota ya jirani Alpha Centauri ni mkubwa mno. Hapa kipimo cha mwakanuru hutumiwa.