Waraka wa pili wa Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka 2Pet)
Agano Jipya

Pande mbili za Papyrus Bodmer VIII, nakala ya zamani zaidi ya 2Pet tuliyonayo.

Waraka wa pili wa Petro ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi[hariri | hariri chanzo]

Siku hizi wataalamu wanakubaliana kukanusha barua hiyo kuwa imeandikwa kweli na Mtume Petro, wakisema ni kitabu cha mwisho kuandikwa katika Agano Jipya (labda huko Roma mwaka 100 hivi B.K.).

Kwa hakika iliandikwa baada ya waraka wa Yuda, kwa sababu inatumia maneno yake mengi.

Inawezekana mwandishi alitumia vilevile maneno ya Petro ambayo sasa yamepotea; kwa vyovyote aliandika kwa mamlaka yake kwa makanisa yote ili kuthibitisha mapokeo.

Mada[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na kupinga uzushi, lengo la barua ni kueleza sababu gani Bwana anachelewa kurudi.

Mafundisho mengine muhimu yaliyomo yanahusu uvuvio wa Roho Mtakatifu juu ya waandishi wa Biblia (Paulo mmojawao), wito wetu wa kushiriki umungu, uwepo wa ulimwengu mpya baada ya huu wa sasa kuangamizwa (2Pet 1:3-11,19 21; 3:8-18).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Tafsiri ya Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

Vinginevyo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili wa Petro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.