2012–2013 mapigano ya Wilaya ya Tana River
Kuanzia Agosti mwaka 2012 hadi Januari mwaka 2013, mfululizo wa mapigano ya kikabila kati ya jamii za Orma na Pokomo kutoka Wilaya ya Tana River nchini Kenya yalisababisha vifo vya watu wasiopungua hamsini na mbili. Ghasia hizo zilikuwa mbaya zaidi za aina yake nchini Kenya tangu virugu wa nchi hiyo wa mwaka wa 2007 hadi mwaka wa 2008, ambao ulisababisha vifo vya watu 118 na zaidi ya 13,500 kuhamishwa makazi yao - zaidi ya 50% ya 13,500 walikuwa watoto, wanawake na wazee.
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Makabila makubwa ya Wilaya ya Tana River ni Wapokomo, ambao wengi wao ni wakulima kando ya Mto Tana, na Orma, wengi wao ni watu wa kuhamahama wanaochunga ng'ombe. [1] Kwa ujumla, wilaya hii ni kavu na unakabiliwa na ukame, na mvua zisizo na uhakika katika msimu wa mvua wa mwezi wa Machi mpaka mwezi wa Mei na kutoka mwezi wa Oktoba-mpaka mwezi wa Desemba. Hali ya anga imesababisha mapigano mengi kati ya wakulima na watu wa wanaohamahama kuhusu upatikanaji wa maji. [2]
Takriban siku kumi kabla ya vurugu vya kikabila tarehe 22 Agosti mwaka wa 2012, jamii ya wa Pokomo waliuawa na watu kutoka jamii ya wa Orma. Katika kulipiza kisasi, jami ya wa Pokomo walivamia makaazi ya wanajamii wa Orma na kuchoma nyumba zaidi ya mia moja. [3]
2012
[hariri | hariri chanzo]Tukio la Agosti 22
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 22 Agosti mwaka wa 2012, kulishuhudiwa tukio mbaya zaidi la mapigano nchini Kenya tangu mwaka wa 2007. Katika ghasia hizo za kikabila Wilaya ya Tana River kati ya vikundi vya jamii ya wa Orma na Pokomo , angalau watu 52 waliuawa. [4] [3] Ghasia hizo zilitokea kusini mashariki mwa Kenya, eneo la Reketa la Tarassa, karibu na pwani kwa takriban kilometre 300 (mi 190) kutoka mji mkuu, Nairobi . [3]
Ghasia hizo za kikabila zilitokana na mzozo wa haki za umiliki wa ardhi ya makabila hayo. Polisi wanaamini kwamba shambulio hilo lilifanywa na watu wa jamii ya wa Pokomo, kuwashambulia wanajamii wa Orma, kufuatia uvamizi wa Orma wa mashamba ya Wapokomo.
Washambuliaji walikuwa na mapanga, upinde na mishale, mikuki na bastola. Wanawake thelathini na mmoja, watoto kumi na mmoja, na wanaume wasita waliuawa kupitia vurugu hizo. Kati ya hao, watu thelathini na wanne walikatwakatwa kwa mapanga hadi kufa, huku watu kumi na wanne wakiteketezwa hadi kufa. [5] Wakenya wengine wanne walifariki baadaye kupitia majeraha waliyopata wakati wa shambulio hilo. [6] Kwa kuongezea, Wapokomo walikamata takriban ng'ombe mia mbili ya wanajamii wa Orma.
Tukio la Septemba
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 7 Septemba, karibu saa 3 asubuhi, watu 12 waliuawa na wanajamii wa Orma. radio ya Capital FM ilisema kwamba polisi na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya walisema mashambulizi yalitokea Tarasaa ambapo nyumba ziliteketezwa, katika kile kinachoaminika kuwa mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa watu wa jamii ya Orma dhidi ya wa. Pokomo.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya walitangaza kuwa zaidi ya ng'ombe 300 na mbuzi 400 walivamiwa na nyumba kuteketezwa. [7]
Mnamo tarehe 10 Septemba, watu 38 waliuawa na wanajamii ya Pokomo, wakiwemo maafisa 9 wa polisi. Waliofariki ni wanaume 16, wanawake watano, polisi tisa na watoto wanane. Maafisa hao ni pamoja na maafisa watano kutoka Kitengo cha Utumishi Mkuu, Polisi wawili wa Utawala na maafisa wawili wa polisi wa kawaida. Vurugu hizo zilitokea katika Kijiji cha Kilelengwani. [8]
Watu watatu waliuawa na wanajamii wa Orma katika vijiji vya Semikaro, Laini, Nduru na Shirikisho vya Tana Delta asubuhi yakufwatia Septemba 11. [9]
Tarehe 13 Septemba, zaidi ya maafisa wa polisi 1300 walitumwa kuzima machafuko huko Mto Tana. [10]
Tarehe Septemba 17, masaa ya 5.45 asubuhi, nyumba 67 ziliteketezwa katika Kijiji cha Ozi, hakukuwa na majeruhi yalioripotiwa. Siku iliyofuata, Mbunge Danson Mungatana alidai kwamba nyumba hizo zilichomwa na Kitengo cha Utumishi Mkuu ya polisi, iliyotumwa hapo awali kutoka Nairobi kuzima ghasia hizo. [11]
Siku hiyo hiyo, polisi walipata wanalo shuku kuwa kaburi la halaiki. Polisi walipewa amri ya mahakama ya kuchimba kaburi lililoshukiwa, lakini walipata sehemu tu ya mguu wa mwanadamu. Mwanachama wa Shirika la Msalaba Mwekundu aliripoti uvundo mkali kutoka eneo hilo. [12]
Tukio la Desemba
[hariri | hariri chanzo]Siku ya Ijumaa, tarehe 21 Desemba mwaka wa 2012, mapigano mapya yakatokea, na ripoti za awali zikionyesha vifo vya zaidi ya watu 27. Uvamizi huo wa kikatili ulifanyika asubuhi kwa masaa machache. [13] Ripoti zilizofuata zilithibitisha mauaji ya watu thelathini na watisa.
Miongoni mwa waliofariki ni washambuliaji ambao maiti zao ziliteketezwa kwa hasira na wakazi. Baada ya mauaji hayo polisi pia waliwakamata zaidi ya washukiwa 65. [14]
2013
[hariri | hariri chanzo]Januari
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 9 Januari mwaka wa 2013, watu kumi na mmoja waliuawa katika mapigano mapya wakati watu wanaoshukiwa kuwa wavamizi wa jamii ya Pokomo waliposhambulia Kijiji cha Nduru na kuua wanajamii wasita wa Orma. Wanakijiji walikabiliana na washambuliaji, na kuwaua wavamizi wawili papo hapo, na wengine wawili walipokuwa wakiwafuata. Mshambuliaji mmoja alifariki kutokana na majeraha alipokuwa akitoroka. [15]
Alfajiri ya tarehe 10 Januari mwaka wa 2013, mashambulizi yalisababisha vifo vya watu 11 katika kijiji cha Pokomo cha Kibusu . [16] Waliokufa ni wanawake watatu, wanaume watatu na watoto watano. [16] Shambulio hilo pia lilisababisha kuchomwa kwa nyumba 19 katika kijiji hicho, ambazo ni takriban kilomita 20 kutoka kijiji cha Nduru kilichoshambuliwa siku moja kabla. [17] Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya pia lilionyesha kuwa zaidi ya watu 112,000 walikuwa wamehamishwa makazi yao tangu ghasia hizo kuanza licha ya kutumwa kwa maafisa 2,000 wa utelekezji wa sheria. [18]
Mwitikio wa serikali
[hariri | hariri chanzo]Msaidizi wa Waziri wa Mifugo na Mbunge wa Galole Dhadho Godhana walikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi, baadae kualiachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Kshs. 500,000. [19]
Siku hiyo hiyo bunge la Kenya lilipitisha hoja ya kuhimiza mtendaji kutuma vikosi vya ulinzi wa Kenya huko mto Tana. Mbunge wa Garsen Danson Mungatana ndiye aliwasilisha hoja hilo . [20]
Uchunguzi wa mahakama
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 22 Septemba, serikali iliunda Tume ya uchaguzi ya mahakama kuhusu mapigano ya Mto Tana, iliyoongozwa na jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka . [21] Wanachama kamili wa tume iliyoteuliwa na Rais Mwai Kibaki ni:
- Lady Justice Grace Nzioka - Mwenyekiti
- Hakimu Mkuu Emily Ominde
- Hakimu Mkuu Abdulqadir Lorot Ramadhan
Wasaidizi wa ushauri ni: [22]
- Bw Wamuti Ndegwa
- Bi Ruth Luta
Miongoni mwa mashahidi walioshuhudia ni: [23]
- Waziri wa ulinzi Yusuf Haji
- Mkuu wa Mkoa wa Pwani Samuel Kilele
- Mkuu wa polisi wa mkoa Aggrey Adoli
- Kamishna wa Ardhi Zablon Mabea
Takwimu za majeruhi
[hariri | hariri chanzo]Ifuatayo ni jedwali la majeruhi ilivyonaswa na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya kufikia tarehe 12 Septemba mwaka wa 2012.
| Tarehe | Kijiji | Vifo | Majeruhi | Mali iliyopotea | Kaya | Idadi ya watu | |||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Mwanaume | Kike | Mtoto | Jumla | Nyumba | Ng'ombe | Mbuzi | |||||
| 14 Agosti | Kau | 2 | 1 | 0 | 3 | 7 | 110 | 198 | 0 | 324 | 1,924 |
| 22 Agosti | Reketa | 6 | 34 | 13 | 53 | 22 | 78 | 60 | 0 | 383 | 2,298 |
| 1 Septemba | Semikaro | 1 | 0 | 0 | 1 | 2 | 0 | 0 | 200 | 0 | 0 |
| 7 Septemba | Chamwanamuma | 15 | 13 | 1 | 17 | 10 | 94 | 200 | 400 | 1,094 | 6,564 |
| 10 Septemba | Kilelengwani | 25 | 5 | 8 | 38 | 8 | 167 | 0 | 0 | 200 | 1,200 |
| Septemba 11 | Laini | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 20 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| Septemba 11 | Sirikisho | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 109 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| Septemba 11 | Semikaro | 4 | 0 | 0 | 4 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| Septemba 11 | Nduru | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 90 | 0 | 0 | 0 | 0 |
| Jumla | 51 | 43 | 22 | 116 | 49 | 668 | 458 | 600 | 2,001 | 12,006 | |
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Weiss, Taya. Guns in the Borderlands (PDF). ku. 89–93. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 29 Septemba 2006. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2012.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tana River District: a showcase of conflict over natural resources". Practical Action. Septemba 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 "Over 50 Kenyans hacked, burned to death: police". Yahoo News. 22 Agosti 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Agosti 2012. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>tag; name "Yahoo" defined multiple times with different content - ↑ "Dozens killed in Kenya clashes". Al Jazeera. 22 Agosti 2012. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑
{{cite news}}: Empty citation (help) - ↑ "Over 50 Kenyans hacked, burned to death: police". 22 Agosti 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2013. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link) CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Cyrus Ombati (10 Septemba 2012). "Police officers among 38 killed in Tana River". Standard Digital News – Kenya. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Three killed in fresh Tana violence". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Standard Digital News. "GSU officers off to clash torn Tana River". Standard Digital News – Kenya. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "MP claims GSU officers razed village in Tana". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "No bodies found in suspected mass grave in Kenya". Capital News. 20 Septemba 2012. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "39 killed in fresh Tana Delta clashes". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tana villagers burn up slain attackers' bodies". Standard Digital News – Kenya. 23 Desemba 2012. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "11 killed in fresh fighting in Tana Delta as DO flees villagers' attack". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 Nyassy, Daniel (10 Januari 2013). "11 killed in Tana revenge attack". Daily Nation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-08-21.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Deadly reprisal raid in Kenya's Tana delta". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "UN condemns 'inhumane' Tana violence". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Minister Godhana arrested over Tana clashes". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "House passes motion to deploy KDF to Tana Delta". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Kibaki appoints commission to probe Tana clashes". Capital News. 22 Septemba 2012. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tana inquiry team commences task". Standard Digital News – Kenya. 2 Oktoba 2012. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "I had no role in Tana clashes, says minister". Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)