Vaginosisi inayosababishwa na bakteria : Tofauti kati ya masahihisho
from English (EN) Wikipedia and Medical Translation Task Force with help from Translators Without Borders (human translation). CC-BY-SA |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 18:26, 11 Machi 2016
Vaginosisi inayosababishwa na bakteria | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Gynaecology ![]() |
ICD-10 | B96., N76. |
ICD-9 | 616.1 |
MeSH | D016585 |
Vaginosisi inayosababishwa na bakteria (BV), hali ambayo pia inajulikana kama bakteriosisi ya uke au Vaginitisi ya gadinerela,[1] ni ugonjwa wa uke unaosababishwa na wingi wa bakteria.[2] Dalili za kawaida ni pamoja na ongezeko la mchozo wa uke ambao mara nyingi hutoa harufu ya samaki. Mchozo huu huwa wa rangi nyeupe au jivu. Kuchomwa na mkojo ni hali inayoweza kutokea.[3] Kuwashwa huwa nadra.[2][3] Mara kwa mara, hali hii huwa bila dalili.[3] Uwepo wa BV huongeza hatari ya maambukizi ya hali nyingine kadhaa za maambukizi ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU/ UKIMWI.[4] Hali hii pia huongeza hatari ya kujifungua mapema miongoni mwa wanawake wajawazito.[5]
Kisababishi na utambuzi
BV husababishwa na ukosefu wa uwiano wa bakteria asilia ukeni.[6] Kuna mabadiliko katika aina ya bakteria inayotokea mara nyingi zaidi na ongezeko la mia hadi elfu moja ya idadi jumla ya bakteria zilizopo.[2] Vipengele vya hatari hujumuisha kupiga bomba, wapenzi wapya au wengi, antibiotiki, na kutumia kifaa cha kuingiza ndani ya uterasi.[6] Hata hivyo, ugonjwa huu hauainishwi kama ugonjwa wa zinaa.[7] Utambuzi hukisiwa kwa msingi wa dalili na unaweza kuthibitishwa kwa kupima mchozo wa uke na kutambua viwango vya juu kuliko kawaida vya pH ya ukeni na idadi kubwa ya bakteria.[2] Mara nyingi BV hudhaniwa kuwa maambukizi ya chachu ya ukeni au maambukizi ya Trikomonasi.[8]
Kinga na matibabu
Kwa kawaida, matibabu huwa ya antibiotiki, clindamycin au metronidazole. Dawa hizi pia zinaweza kutumika katika trimesta ya pili au ya tatu ya ujauzito. Hata hivyo, mara nyingi hali hii hurejea baada ya kutibiwa. Probiotiki zinaweza kusaidia kuzuia kurejea kwa hali hii.[2] Haijulikani bayana kama kutumia probiotiki au antibiotiki huathiri matokeo ya ujauzito.[2][9]
Epidemiolojia na historia
BV ni maambukizi ya uke yanayotokea mara nyingi katika wanawake wa umri wa kuzaa.[6] Idadi ya wanawake wanaoathiriwa katika muda fulani ni kati ya asilimia 5 na asilimia 70.[4] BV hutokea mara nyingi zaidi katika maeneo mengi ya Afrika na ni nadra barani Asia na Ulaya.[4] Nchini Marekani, takriban asilimia 30 ya wanawake wa umri wa kati ya miaka 14 na 49 huathiriwa.[10] Viwango hutofautiana sana katika makundi ya kikabila mbalimbali katika nchi.[4] Ingawa BV kama dalili imeainishwa katika kipindi kirefu cha historia, nakala za kwanza bayana ziliwekwa katika mwaka wa 1894.[1]
Marejeo
- ↑ 1.0 1.1 (1997) Sexually transmitted diseases : epidemiology, pathology, diagnosis, and treatment. Boca Raton [u.a.]: CRC Press, 4. ISBN 9780849394768.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Donders, GG; Zodzika, J; Rezeberga, D (April 2014). "Treatment of bacterial vaginosis: what we have and what we miss.". Expert opinion on pharmacotherapy 15 (5): 645-57. .
- ↑ 3.0 3.1 3.2 What are the symptoms of bacterial vaginosis? (05/21/2013). Iliwekwa mnamo 3 March 2015.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 Kenyon, C; Colebunders, R; Crucitti, T (December 2013). "The global epidemiology of bacterial vaginosis: a systematic review.". American journal of obstetrics and gynecology 209 (6): 505-23. .
- ↑ What are the treatments for bacterial vaginosis (BV)? (07/15/2013). Iliwekwa mnamo 4 March 2015.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 Bacterial Vaginosis (BV): Condition Information (05/21/2013). Iliwekwa mnamo 3 March 2015.
- ↑ Bacterial Vaginosis – CDC Fact Sheet. Centers for Disease Control and Prevention (March 11, 2014). Iliwekwa mnamo 2 Mar 2015.
- ↑ Mashburn, J (2006). "Etiology, diagnosis, and management of vaginitis.". Journal of midwifery & women's health 51 (6): 423-30. .
- ↑ Othman, M; Neilson, JP; Alfirevic, Z (24 January 2007). "Probiotics for preventing preterm labour.". The Cochrane database of systematic reviews (1): CD005941. .
- ↑ Bacterial Vaginosis (BV) Statistics Prevalence (September 14, 2010). Iliwekwa mnamo 3 March 2015.