Mpangilio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mpangilio ni utaratibu maalumu wa kupanga maneno au mambo ili kuunda sentensi ambazo zinatoa maana na kupendeza, kurahisisha utafutaji, n.k. Kwa sababu hiyo ni tofauti na orodha ambayo mara nyingi hufuata alfabeti tu. Kwa namna nyingine, mpangilio ni mtiririko wa mambo au mawazo kwa utaratibu unaoeleweka au unaotakiwa.