Ziwa la Nasser
| Lake Nasser | |
|---|---|
| View from Abu Simbel | |
| Ramani inayo onyesha eneo la ziwa | |
| Aina ya ziwa | Kiegezo |
| Mito ya kuingia | Nile |
| Mito ya kutoka | Nile |
| Nchi za beseni | Egypt, Sudan |
| Urefu | 550 km (340 mi) |
| Upana | 35 km (22 mi) |
| Eneo la maji | 5,250 km2 (2,030 sq mi) |
| Kina cha wastani | 25.2 m (83 ft) |
| Kina kikubwa | 180 m (590 ft) |
| Mjao | 132 km3 (51,000 sq mi)[1] |
| Urefu wa pwani (km) | 7,844 km (25,735,000 ft) |
| Kimo cha uwiano wa maji uso juu ya UB | 183 m (600 ft) |
| Marejeo | [1] |
| 1 Shore urefu is not a well-defined measure. | |
Ziwa la Nasser (Kiarabu بحيرة ناصر buhairat nāssir) ni bwawa kubwa kwenye mto Nile iliyopatikana tangu kufungwa kwa mwendo wa Nile kwa lambo la Aswan nchini Misri kuanzia mwaka 1958.
Ziwa Nasser liko katika eneo la nchi za Misri na Sudan, hasa kati ya miji ya Aswan (Misri) na Wadi Halfa (Sudan). Eneo lake ni zaidi ya 5,200 km² lina urefu wa kilomita 550 km na upana hadi 35 km. Mjao hufikia hadi 160 km³.
Jina lilitolewa kwa heshima ya aliyekuwa rais wa Misri Gamal Abdel Nasser aliyefanya azimio la kujenga bwawa.
Faida na matatizo ya ziwa [hariri]
Kuzuiliwa kwa mwendo wa mto ulimaliza mafuriko ya kila mwaka ya Nile nchini Misri. Kwan upande mwingine matope yenye rutba hayafiki tena chini ya Aswan na wakulima wahitaji kununua mbolea wa chumvi waliporidhika zamani na matope yaliyobaki mashambani baada ya mafuriko. Vilevile matope haya yameanza kujaza nafasi ya ziwa na mjao wake umeendelea kupungua polepole.
Pia delta ya Nile katika Mediteranea haikukua tena lakini imeanza kupungukiwa.