Zaire (mkoa)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zaire ni jina la mkoa wa kaskazini-magharibi nchini Angola mwenye eneo la 40,130 km² na wakazi 600,000.
[hariri] Mipaka
Mkoa umepakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoitwa "Zaire" hadi 1997. Mipaka mingine ni mikoa ya Uige upande wa mashariki, Cuanza Norte upande wa kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi.
[hariri] Miji
Makako makuu ni mji wa M'banza-Kongo. Miji mingine ni Soyo kwenye mdomo wa mto Kongo, Tomboco, N'Zeto kwenye mdomo wa mto Mebridege na Noqui kando la Matadi kwenye mpaka wa Kongo.
[hariri] Uchumi
Uchumi ni hasa kilimo na uvuwi pamoja na migodi, kuchimba madini na mafuta ya petroli.
