Zachary Onyonka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zachary Onyonka

Zachary Onyonka (1938 - 2002) alikuwa mwanasiasa wa Kenya. Alikuwa mbunge, akiwakilisha Eneo bunge la Kitutu Masaba.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Onyonka alizaliwa mnamo 1938 katika sehemu za Kisii nchini Kenya.

Ubunge[hariri | hariri chanzo]

Alichaguliwa mara ya kwanza kama mbunge wa Kitutu West wakati jimbo hili lilipoanzishwa mnamo 1969. Abakia kuwa mbunge wa Jimbo hili la uchaguzi hadi 1988 wakati jimbo hilo liligawanywa na kuzaa jimbo jipya la Kitutu Chache. Onyonka alikuwa mbunge wa jimbo hili jipya hadi kifo chake mnamo 2002.

Uwaziri[hariri | hariri chanzo]

Onyonka alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje kati ya 1987 - 1988.

Kifo chake[hariri | hariri chanzo]

Aliaga dunia mnamo 2002 wakati angali akihudumu kama mbunge wa Kitutu Chache.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Alitanguliwa na
Elijah Mwangale
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya
1987-1988
Akafuatiwa na
Robert Ouko (mara ya pili)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zachary Onyonka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.