Yosefu wa Kopertino
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yosefu wa Copertino Picha kutoka kitabu cha Paul Guerrin, "Les Petites Bollandistes: Vies de Saints," 1882.
Yosefu wa Kopertino (Copertino 17 Juni 1603 – Osimo 18 Septemba 1663) alikuwa padri wa utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali.
Mtu wa sala hasa, alijaliwa karama za pekee, hasa ile ya kuelea hewani kwa muda mrefu wakati wa kutoka nje ya nafsi.[1]
Alitangazwa na Papa Benedikto XIV kuwa mwenye heri tarehe 24 Februari 1753, halafu Papa Klement XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767.
Tanbihi [hariri]
- ↑ "Saint Joseph of Copertino," Fr. Angelo Pastrovicchi, O.M.C., TAN Books and Publishers, 1980, p. iii
Marejeo [hariri]
- "Saint Joseph Copertino," Father Angelo Pastrovicchi, O.M.C., TAN Books and Publishers, 1980, ISBN 0-89555-135-7