Yohane wa Dameski
Yohane wa Dameski (kwa Kiarabu يوحنا ابن ﺳﺮﺟﻮﻥ Yuḥannā ibn Sarjūn) alikuwa mmonaki, padri na mwanateolojia kutoka Dameski mji mkuu wa Siria (676? - 749?).
Anaheshimiwa kama mtakatifu, babu wa Kanisa na mwalimu wa Kanisa. Ni msimamizi wa wachoraji.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 4 Desemba.
[hariri] Maisha
Alizaliwa katika familia ya Kiarabu ya Kikristo. Baba yake alikuwa Sarjūn ibn Manṣūr. Babu yake, Manṣūr, alikuwa wa kwanza katika familia kupewa vyeo vikubwa chini ya utawala wa halifa Mu'awiya bin Abi Sufyan na wa waandamizi wake.
Alipokuwa kijana alipata kuwa mshauri wa halifa wa Damasko na msimamizi wa mali.
Lakini baadaye akahukumiwa na kukatwa mkono wa kushoto. Hapo alihama mji huo na kujiunga na monasteri ya Mt. Saba, kati ya Bethlehemu na Yerusalemu, ambapo alifanya askofu.
Alihubiri na kuandika sana hadi kifo kilipompata akiwa na umri wa miaka 73.
Kitabu chake maarufu zaidi kinaitwa Kuhusu Imani Sahihi.
Alitumia nguvu zake zote hasa kutetea sanamu katika Ukristo. Alipewa ushindi na Mtaguso wa pili wa Nisea (787) baada ya kifo chake.
[hariri] Vyanzo
- (2003) The rise of Western Christendom: triumph and diversity, A.D. 200-1000, 2nd, illustrated, Wiley-Blackwell.
- (2000) Butler's lives of the saints: Volume 12 of Butler's Lives of the Saints Series, Revised, Continuum International Publishing Group.
- Jameson (2008). Legends of the Madonna. BiblioBazaar, LLC.
- (2002) St. John Damascene: tradition and originality in Byzantine theology, Illustrated, Oxford University Press.
- (2004) Fifty key Christian thinkers. Routledge.
- (1972) John of Damascus on Islam. BRILL.
- (2000) in Richard Valantasis: Religions of late antiquity in practice, Illustrated, Princeton University Press.
- (1997) The Works of St. John Damascene. Martis Publishing House, Moscow.
[hariri] Viungo vya nje
- Maandishi yake yote pamoja na faharasa katika Patrologia Graeca ya Migne
- 131 Christians Everyone Should Know- John of Damascus
- Catholic Encyclopedia: St. John Damascene
- Britannica Concise Encyclopedia
- Catholic Online Saints
- Details of his work
- Excerpt from John Damascene
- "Apologia Against Those Who Decry Holy Images" at the Internet Medieval Sourcebook
- A Philosophical Explanation of Hypostatical Union in John Damascene's Fount of Knowledge
- The Concept of Unbounded and Evil Matter in Plotinus and John Damascenus
- Works by John of Damascus katika Project Gutenberg
- "St. John of Damascus' Critique of Islam" at the Orthodox Christian Information Center
- Greek Opera Omnia by Migne, Patrologia Graeca with Alaytical Indexes
- St John of Damascus Orthodox Icon and Synaxarion (December 4)