Yairo (Injili)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Yairo)
Ufufuo wa Binti Yairo kadiri ya Paolo Veronese, 1546.

Yairo ni maarufu kama baba wa msichana aliyefufuliwa na Yesu Kristo kama inavyosimuliwa na Injili ndugu (Mk 5:21–43; Math 9:18–26; Lk 8:40–56).

Kiongozi wa sinagogi fulani, alikuwa amemkimbilia kwa imani Yesu kwa ajili ya binti yake.

Walipofika nyumbani walikuta msiba umeshaanza, lakini Yesu alifukuza waombolezaji, akamfufua mtoto huyo wa miaka 12 mbele ya Yairo mwenyewe, mke wake, Petro, Yakobo Mkubwa na Yohane tu.

Hatimaye aliagiza binti apewe chakula.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yairo (Injili) kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.