With You (nyimbo ya Chris Brown)
| “With You” | |||||
|---|---|---|---|---|---|
![]() |
|||||
| Single ya Chris Brown kutoka katika albamu ya Exclusive |
|||||
| Imetolewa | Marekani 4 Desemba, 2007 Uingereza 24 Machi, 2008 |
||||
| Muundo | CD | ||||
| Imerekodiwa | 2007 Battery Studios (New York City, New York) |
||||
| Aina | Pop/R&B | ||||
| Urefu | 4:11 | ||||
| Studio | Jive, Zomba | ||||
| Mtunzi | Johntá Austin, Tor Erik Hermansen, Mikkel Eriksen, Espen Lind, Amund Bjørklund | ||||
| Mtayarishaji | Stargate | ||||
| Mwenendo wa single za Chris Brown | |||||
|
|||||
| Kasha badala | |||||
Kasha ya Australia, Ufaransa na Ufalme wa Muungano
|
|||||
"With You" ni nyimbo ya pop na R&B ya mwanamuziki Chris Brown, imetungwa na Johntá Austin, Tor Erik Hermansen, Mikkel Eriksen, Espen Lind na mwisho kabisa Amund Bjørklund.
Nyimbo ilitayarishwa na Bw. Stargate ambaye pia alitayarisha nyimbo ya "Unfaithful" na "Hate That I Love You" ya Rihanna na "Irreplaceable" ya Beyonce Knowles. Nyimbo imetoka ikiwa kama single ya tatu kutoka katika albamu ya pili ya Brown ijulikanayo kwa jina la Exclusive ya mwaka wa 2007.
Wapenzi wengi wa muziki walikuwa wakiponda nyimbo hiyo kwa madai ya kwamba nyimbo inafanana sana na ile ya Beyonce (Irreplaceable), ingawaje Chris na Stargate hawajapata pigo lolote juu ya nyimbo hiyo.
Kufuatia kuto fanya vizuri katika vhati nyimbo yake ya "Wall To Wall" na "Kiss Kiss", "With You" ikatoka mnamo tar. 4 Desemba, 2007 katika albamu zake za Marekani, na ikawa nyimbo yake ya pili kupata mafanikio katika soko la muziki la kimataifa.
[hariri] Marejeo
- United World Chart Media Traffic. Accessed March 27, 2008.
- Chris Brown With You review About.com. Accessed January 20, 2008.

