Wilaya ya Tharaka
Wilaya ya Tharaka ni moja kati ya Wilaya 71 za Kenya.
Yaliyomo |
Jiografia [hariri]
Wilaya hii inapatikana katika Mkoa wa Mashariki wa Kenya. Ina Ukubwa wa ardhi wa 1570 kmВ
Idadi ya Wakazi [hariri]
Idadi ya watu katika Wilaya hii kulingana na Hesabu ya 1999 ni 100,992[1], na hakuna wanaohesabiwa kuwa wakazi wa Mtaani. Mnamo 1998, Wilaya hii ilitenganishwa kutoka Tharaka-Nithi[2], ambayo pia ilikuwa sehemu ya Wilaya Kubwa ya Meru.
Wakazi [hariri]
Tharaka ndiyo maskani ya watu wa Ameru (Wameru) ambao wakati mwingine wanatajwa kuwa na uhusiano na kabila zingine ziishizo katika maeneo ya Mlima Kenya: Wakikuyu na Waembu. Wameru ni Wabantu, watu ambao wameishi kando ya Mlima Kenya kwa miaka mingi, hata kabla ya Ukoloni.
Dini [hariri]
Watu wa Tharaka wengi ni wa dini ya Kikristo (Methodist, Presbyterian na Roman Catholic), ikiashiria kazi ya Wamishonari. Wengine ni Wahindi, ambao dini yao ni Hindu. Pia kuna Waafrika na Waarabu ambao ni Waislamu. Tharaka pia ina baadhi ya wakazi wa asili ya Kizungu
Utawala [hariri]
Makao Makuu [hariri]
Makao makuu ya wilaya hii ni Tharaka (Marimanti).
Mabaraza ya Mitaa [hariri]
Tharaka ina baraza moja tu, Tharaka County
Majimbo ya Uchaguzi [hariri]
Pia ina Jimbo moja la uchaguzi, Tharaka.
Tarafa za Utawala [hariri]
| Tarafa za Utawala | |||
| Tarafa | Idadi ya wakazi* | Makao Makuu | |
|---|---|---|---|
| Tharaka ya Kati | 38,914 | Marimanti | |
| Tharaka Kaskazini | 36,904 | Gatunga | |
| Tharaka Kusini | 25,174 | Chiakariga | |
| Jumla | 100,992 | - | |
| * 1999 census. Viini: [1], [2], | |||
Virejeleo [hariri]
- ↑ statoids.com û Districts of Kenya
- ↑ Sheila Aikman, Elaine Unterhalter: Beyond access: transforming policy and practice for gender equality in education. Oxfam, 2005
Viungo vya Nje [hariri]
Anwani ya kijiografia: 0°18′S 38°0′E / 0.3°S 38°E
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mashariki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Tharaka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |