Wilaya ya Gucha
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gucha ni wilaya katika Mkoa wa Nyanza, magharibi mwa Kenya. Hujulikana pia kwa jina: Wilaya ya Kisii Kusini au Wilaya yaOgembo. Wakazi wake ni takriban 461,000 (kama ilivyo 1999) [1] Makao yake makuu yako Ogembo iliyo na wakazi zaidi ya elfu moja, (watu ambao wanaishi katikati mwa mji), na zaidi ya watu elfu moja huitembelea kila siku. Kilimo ndio sekta kuu. Bali mashamba mengi madogo madogo, kuna mashamba makubwa ya miwa. Idadi ya watu wengi ni Wakisii, lakini hupakana na ardhi ya masai huko kusini-mashariki. Kumekuwa na mapigano kadha ya kikabila baina yao.
Wilaya hii ina majimbo matatu: South Mugirango, Bomachoge na Bobasi. Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2002 viti vyote vitatu vilishindwa na chama cha Ford-People.
| Mamlaka za Mitaa (Halmashauri) | |||
| Mamlaka | Aina | Idadi ya Watu | Wakazi wa mjini* |
|---|---|---|---|
| Ogembo | Jiji | 48.725 | 1.654 |
| Nyamarambe | Jiji | 40.232 | 212 |
| Nyamache | Jiji | 38.924 | 2.205 |
| Tabaka | Jiji | 26.325 | 5.067 |
| Gucha | County | 306.733 | 1.946 |
| Jumla | -- | 460.939 | 11.084 |
| * 1999 census. Source: [2] | |||
| Maeneo ya utawala | |||
| Tarafa | Idadi ya Watu | Wakazi wa mjini* | Makao makuu |
|---|---|---|---|
| Etago | 59.652 | 0 | |
| Kenyenya | 92.641 | 1.857 | |
| Nyacheki | 56.998 | 405 | |
| Nyamache | 54.722 | 1.702 | |
| Nyamarambe | 67.060 | 3.850 | |
| Ogembo | 78.827 | 1.465 | Ogembo |
| Sameta | 51.039 | 0 | |
| Jumla | 460.939 | 9.279 | -- |
| * 1999 census. Sources: [3], [4], | |||
Viungo vya nje [hariri]
- Lugha
- Lugha ya Kisii - Kisii Utafsiri wa Kiingereza-Ekegusii
| Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Gucha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |