Uvuvi
Uvuvi ni kazi ya kukamata samaki na pia ufugaji wa samaki na wanyama wengine wa maji. Kusudi lake ni hasa kupata chakula lakini siku hizi uvuvi unatokea pia kama burudani, katika utalii na kama sehemu ya michezo.
Uvuvi ni kati ya shughuli za kale kabisa za binadamu na katika uchumi huhesabiwa katika sekta ya msingi pamoja na kilimo na uchimbaji wa madini. Kutokana na takwimu za FAO kuna watu milioni 38 dunani wanaofanya kazi ya kuvua au kufuga samaki. Pamoja na wengine wanaosafirisha windo na kulifanyia kazi viwandani au kuiuza masokoni, madukani au kwenye hoteli kuna zaidi ya watu 500 wanaopata maisha yao na sekta hii ya uvuvi. [1]
Uvuvi hufanywa penye magimba ya maji kama kwenye bahari, maziwa, mito au mabwawa. Mara nyingi wavuwi hutumia chombo cha maji kama boti lakini wengine wanakaa ufukoni na kuvua kutoka nchi kavu.
Vyombo vya uvuvi ni aina za nyavu zinazoweza kushika samaki yote na kuivuta nje ya maji, ndoano au pia aina za mikuki inayolenga samaki zilizipo karibu na uso wa maji.
Marejeo [hariri]
- ↑ ftp://ftp.fao.org/FI/brochure/climate_change/policy_brief.pdf Fish (including shellfish) provides essential nutrition for 3 billion people and at least 50% of animal protein and minerals to 400 million people in the poorest countries. • Over 500 million people in developing countries depend, directly or indirectly, on fisheries and aquaculture for their livelihoods. • Aquaculture is the world’s fastest growing food production system, growing at 7% annually. • Fish products are among the most widely traded foods, with more than 37% by volume of world production traded internationally.