Watumishi wa Maria
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utawa wa Watumishi wa Maria, kwa Kilatini Ordo Servorum Beatae Virginis Mariae (kifupi O.S.M.), ni shirika la maisha ya wakfu aina ya ombaomba katika Kanisa Katoliki.
Ulianzishwa Firenze (Italia) mwaka 1233 hivi, na kundi la waamini maarufu kama waanzilishi saba watakatifu.
Katika lebo ya shirika "S" (Servi) inaendana na "M" (Maria). Taji linaundwa na maua saba, yanayowakilisha waanzilishi wake watakatifu.]]