Wati
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wati (pia:watt) ni kizio cha kupima nguvu. Kifupi chake ni W. Fomula yake ni kg·m2·s−3.

Inaelezwa kuwa ni nguvu inayotokea kama juli moja ya nishati inatumiwa kwa muda wa sekunde moja. Hivyo inawezekana kuiandika pia kama J/s.
Wati moja ni sawa na volti-ampea moja (1 V·A).
Wati ni kizio cha vipimo sanifu vya kimataifa. Imepewa jina lake kwa heshima ya mwanafizikia na mhandisi James Watt (1736 - 1819).
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
.